Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ELIMIKA

 

Umuhimu wa lishe bora kwa watoto wetu.






Maana.

Chakula ni kitu ambacho watu ama wanyama wanakula na mimea inafyonza ili kuleta na kuwezesha uhai.

Hivyo chakula ni lishe. Afya bora inatokana na mpangilio mzuri wa ulaji wa chakula. Hapa ni muhimu kuzingatia uwiano mzuri wamakundi ya vyakula na muda wa milo.

Mara nyingi watu katika nchi zetu hizi maskini zinazojikwamua kimaendeleo wanakumbwa na matatizo yanayosababishwa na ulaji wa chakula usiozingatia mpangilio ama uwiano mzuri wa makundi ya vyakula. Lakini hii inasababishwa na umaskini, njaa hasa inayosababishwa na hali mbaya ya hewa, ukame na miundombinu mibovu ya nchi yetu.

Katika nchi zetu zinazoendelea watoto wengi na wazee wanaonekana kuwa na utapiamlo (malnutrion). Ukijionesha kupitia unyafuzi na kwashakoo.



Umuhimu wa chakula.

Tunakula chakula ili kuondoa njaa na kuupa mwili virutubisho vya kuufanya uendelee kuwa na nguvu na afya bora. Chakula lazima kiwe safi na salama na kinatakiwa kiwe cha kutosha kulingana na umri, kazi na hali ya mtu. Ubora wa chakula pia hutegemea upatikanaji wa virutubisho vyote, yaani wanga, protini, mafuta, maji, madini na vitamini.



Madhara ya lishe duni.

Madhara yafuatayo husababishwa na kutokuzingatia lishe bora kwa watoto.

  • Utapiamlo.(malnutirion)

  • Kiribatumbo.

  • Kwashakoo.

-Unyafuzi. (kwashiorkor)



Unyafuzi husababishwa na ukosefu wa virutubisho vya aina ya protini kama mayai, nyama n.k. Hali hii hutokea sana kwa watoto kwa kukosa chakula bora kwa kupata vyakula vya wanga sana na kula protini kidogo.





Dalili.

  • Kupungua uzito.

  • Nywele za rangi ya shaba na dhaifu.

  • Tumbo kubwa.

  • Kuvimba kwa uso na miguu.

  • Kukosa hamu ya kula.

-Nyongea. (rickets)

Nyongea husababishwa na kukosekana kwa wanga na mafuta ya kutosha katika chakula.






Dalili.

  • Upungufu mkubwa wa uzito.

  • Kuzeeka kwa sura.

  • Kwa watoto hutaka kula wakati wote.

  • Macho meupe.

-Kiribatumbo.



Kiribatumbo husababishwa na kuzidi mafuta mwilini. Kiribatumbo huambatana na maradhi kama vile ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu.



-Rovu. (goitre)



Rovu husababishwa na ukosefu wa madini joto/iodine mwilini. Rovu hujitokeza kwa kuvimba tezi za shingo. Pia kudumaa kwa akili na mwili hutokea.






-Upungufu wa damu. (nutritional anaemia)

Upungufu wa damu ama uwekundu wa damu husabisha udhaifu wa mwili, kuchoka mara kwa mara, kusinzia na kuhema haraka haraka. Tatizo hili usababishwa na upungufu wa madini chuma (iron). Mboga za majani, matunda na nyama hutatua tatizo hili.



Ni muhimu sana kwa watoto kupatiwa lishe bora ikiwa ni haki yao ya msingi kuishi kwa afya bora, ewe mzazi licha ya kuwa una maisha duni jitahidi sana kulisha mtoto au watoto wako vizuri.Magonjwa haya yanaweza kuzuilika kabisa kama utazingatia lishe sahihi na iliyo bora kwa mtoto/watoto wako. Kama huna hela ya kununua vyakula vya gharama, unaweza kutafuta au kununua vyakula mbadala vyenye bei ndogo lakini ni vyenye thamani kubwa ya virutubisho katika mazingira unayoishi. Ukigundua mtoto wako ana dalili za ugonjwa unaotokana na ukosefu wa lishe bora, nenda kliniki au zahanati iliyokaribu na mahali unapoishi kupata tiba ya mtoto pamoja na ushauri wa lishe bora ya mwanao.

SOMO LA KWANZA LA DIGITALI: MAWASILIANO YA SATELITE


Picha ya Satelite aina ya SPUTNIK 1 
MAWASILIANO YA SATELAITI 

Satelaiti ni nini?  
Nikifaa (mashine au mtambo) ambao huwekwa angani kuzunguka dunia au kitu chochote kilichoko angani.


 
Satelaiti ya kwanza kutengenezwa na binadamu, kupelekwa angani na kuwekwa katika obiti kuzunguka dunia iliitwa 
 
 SPUTNIK 1.
Ilitengenezwa na Urusi na kupelekwa angani tarehe 4 Octoba, 1957. Satelaiti hii ilisafiri kwa mwendo wa kilomita 29,000(km) kwa saa ikitumia dakika 96.2 kukamilisha mzunguko wa dunia. Ikiwa angani ilituma mawimbi ya mawasiliano katika masafa ya 20.002MHz na 40.002MHz ambayo yalipokelewa na mitambo ya redio za amateur “amateur radio” duniani kote. Iliendelea kutuma mawimbi kwa siku 22 baadaye nguvu ya betri za transmita hizo ziliisha nguvu tarehe 26 Octoba, 1957. Satelaiti hiyo ilianza kudondoka toka katika obiti angani na kuungua tarehe 4 Januari, 1958 baada ya kuingia kwenye anga ya dunia (atmosphere). Ilikaa katika obiti kwa muda wa miezi mitatu.

Kuna satelaiti za aina ngapi?
 
Kuna satelaiti za aina mbili: 

1.      Satelaiti za asili (Natural satellites) mfano; Dunia (Dunia huzunguka Jua) na Mwezi (mwezi huzunguka Dunia).

 
2.      Satelaiti za kutengenezwa na Binadamu (Artificial satellites).


Kuna aina ngapi za Satelaiti za kutengenezwa na binadamu?

Zipo satelaiti za aina nyingi na zimetengwa kwa matumizi mbalimbali.

1.      Satelaiti kwa ajili ya utafiti na uchunguzi sayari za mbali, galaxies na vitu vingine vinavyoelea angani (Astronomical satellites).
 
2.      Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kufanya mawasiliano (Communications Satellites).
 
3.      Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kuangalia hali ya hewa (Weather Satellites).
4.      Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya matumizi ya Ki-intelijensia na Kijeshi (Intelligence and Military Operations Satellites).
 
5.      Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kufanya utafiti wa dunia na vitu vingine vilivyoko angani mfano (Biosatellites ambazo hubeba viumbe hai kwenda angani kwa ajili ya utafiti).
 
6.      Satelaiti zinazowekwa angani kwa ajili ya kufuatilia mabadiliko ya dunia na mazingira (Earth Observational Satellites).
 
7.      Ofisi za uchunguzi wa anga zinazoelea angani (Space Stations).
 
8.      Vifaa (mitambo) vyote vinavyokuwa angani katika obiti (Manned Spacecrafts / Spaceships).
 
9.      Satelaiti ndogo zinazounganishwa katika satelaiti nyingine kwa waya mwembamba unaoitwa tether (Tether Satellites)
 
10.  Satelaiti kwa ajili ya kutambua (mahali/ sehemu) katika uso wa dunia (positioning satellites) mfano GLONASS ni mfumo wa Urusi, GPS (Global Positioning System) ni mfumo wa Marekani, GALILEO ni mfumo wa Ulaya (European Union), China mfumo wao COMPASS (Compass Navigation System).

Satelaiti tunazozitumia kupokea mawimbi ya televisheni / redio zipo katika kundi la Satelaiti za Mawasiliano (Communication Satellites).



Satelaiti hizi za mawasiliano tunazozitumia kupitisha mawasiliano ya televisheni na redio (zipo katika Geosynchronous Orbit) umbali wa kilomita 35,786km kutoka ardhini katika Ikweta na husafiri kwa kasi sawa na kasi ya dunia.


MAWASILIANO KUTOKA SATELAITI ZA MAWASILIANO ZILIZOPO KATIKA "GEOSYNCHRONOUS ORBIT"

KUTAFUTA CHANELI MBALIMBALI ZA TELEVISHENI / REDIO KUTOKA KATIKA SATELAITI MBALIMBALI ZA MAWASILIANO ZILIZOPO KATIKA GEOSYNCHRONOUS ORBIT ; OBITI AMBAYO KWA MAJINA MENGINE HUITWA (PARKING ORBIT au CLARKE BELT au GEOSYNCHRONOUS ARCH)

Kwa kuwa dunia ina umbo la duara si rahisi watu wote tulioopo katika uso wa dunia (namaanisha mabara yote) tukatumia satelaiti moja kupokea mawasiliano toka katika satelaiti. Kusema hivi namaanisha mfano satelaiti tunayoitumia sana (IS 906 @ 64.2E (nyuzi za longitudo 64.2 Mashariki mwa Greenwich) katika ukanda wetu Tanzania ikiwemo haiwezi kufikisha mawimbi yake Marekani kwa sababu Marekani wanakuwa upande mwingine wa uso wa dunia (they are below the horizon of the reach of that satellite) hii ni vile vile kwa satelaiti zinazoimulika Marekana hata sisi hatuwezi kupata mawimbi yake. Mfano baadhi ya satelaiti za Intelsat (IS 902, IS 906, IS 904, IS 10, IS 17, IS 907 na nyinginezo zilizoko juu ya usawa wa Afrika na bahari ya Hindi na wao wakitaka kupokea mawasiliano yake wanatumia kituo chao (kilichopo Afrika Kusini).

Baadhi ya satelaiti ambazo mawimbi yake yanafika hapa Tanzania zipo kati ya nyuzi za longitudo 27 Magharibi mwa Mstari wa Greenwich na nyuzi za longitudo 85 Mashariki mwa Mstari wa Greenwich. Dishi linalozunguka (horizon to horizon) linaweza kupata chaneli mbalimbali kutoka satelaiti hizi kwa kuzunguka kupitia satelaiti moja baada ya nyingine (from 27 West to 85 East). Kadri unavyoelekea Magharibi ndivyo utakavyozidi kupata satelaiti zilizopo Magharibi huku ukipoteza za Mashariki; na kinyume chake (and vice versa).

Baadhi ya satelaiti ambazo zinazunguka kwa kasi sawa na kasi ya dunia; ambazo zipo katika "Geosynchronous Orbit or Parking Orbit" zinazopatikana katika eneo letu (Tanzania na nchi za jirani zimeorodheshwa chini. Satelaiti hizi hutumika kwa mawasiliano mbalimbali mfano Data /Internet, Televisheni, Radio, Mawasiliano ya Ki-intelijensia, kijeshi na mawasiliano mengine.

Intelsat 907 @ 27.5W:
VoA TV, Alhurra TV Iraq, Alhurra TV Europe, RTG (Guinea),
Intelsat 905 @ 24.5W: Nile Drama, Syria 1,

SES 4 @ 22W:
Bolivia Mux,

NSS7 @ 20W: 
CNN, TBN, Emmanuel TV),

Intelsat 901 @ 18W
: Ethiopia Educational Media Agency

Telstar 12 @ 15W:


Nilesat 102 @ 7W: DW Arabia, BBC Arabic, Abu Dhabi, Abu Dhabi Sport 1, Dubai Sport 2, DM    TV, National Geographic Channel,

Intelsat 10 - 10W @ 1W:
 BBC World Service, RTS1 (Senegal)

Rascom QAF 1R @ 2.8E: 
Libya Satellite TV, Libyan Mux, RTNC, Digital Congo (Congo)

Eutelsat 7A @ 7E: Record Mozambique, MBC 1, MBC 2, CRTV, RTS 1 (Senegal), BBC Persian,
ORTM, Raha Tv, TPA Internacional, VoA TV Persian.

Eutelsat 10A @ 10E: 
Startimes, Agape TV Network,

Amos 5 @ 17E:
 Zambia Mux, Reuters Live, Doordarshan, Kingdom Africa TV, Bible Exploration TV, Fashion TV Europe,

Eutelsat 36A @ 36E:
TING Channels (Tanzania), NTV Plus, Afrique TV,

Eutelsat 36B @ 36E:
CCTV News, CCTV 4 Europe, Multichoice DStv channels

NSS 12 @ 57E:         ZUKU, KBC- Kenya, Family TV - Kenya, ETV (Ethiopia), VoA TV Africa, Ameican Embassy tv Network etc.), 


Intelsat 904 @ 60E:  Uganda Mux, Kenya Mux, NTV (Kenya), KBC Channel 1 (Kenya), TBC 1, NTV Uganda (Kenya), Swazi TV, ZNBC,

Intelsat 902 @ 62E:
NTV (Kenya), Citizen TV (Kenya), SABC 1 - 3 (South Africa), Sky News International,

Intelsat 906 @ 64.2E: ITV, EATV, CAPITAL, TBC, STARTV, TVM (Mozambique), UBC (Uganda), Chanel 10,


Intelsat 906 @ 64.2E inakofikisha Mawimbi yake katika masafa ya C Band (Hemi, Zonal & Global Beams)

Intelsat 17 @ 66E:  HMTV, Captain TV, ABN (India), V6 News,

Intelsat 20 @ 68.5E: Indiasign, NHK World TV (Japan), Peace TV Bangla, India TV, South Korea Mux, CTS (South Korea), Hope TV India, YTN World, VTV (India), Peace TV, God TV Africa, Africa Unite TV, ABN (Nigeria), Messiah TV, Citizen TV (Kenya), UB (South Africa), Emmanuel TV, CTV, 3ABN International, Press TV, CCTV,
EWTN, 
Intelsat 7 @ 68.6:     Vivid, UNISA (South Africa), Botswana TV, SABC 1-3, ITV (South Africa France 24 English, God TV Africa, Multichoice South Afica, 
Eutelsat 70A:            Canadian Forces Radio & TV,   ABS 1 @ 75E:

Apstar 7 @ 765E:      ERT World, Channel 9 (Bangladesh), God Asia, 

Thaicom 5 @ 785E:    Somalia National TV, TV5 Cambodia, T Sports Channel, Shop Thailand, Spring.TV News, MRTV,  na nyinginezo. 
Express MD1 @ 80E:

Dishi linaloweza kufanya kazi hii vizuri ni la kipenyo kuanzia futi nane 8ft, 10ft, 12ft na kuendelea (hasa kuanzia futi kumi 10ft na kuendelea).
Kwa madishi ambayo hayazunguki (fixed satellite dishes) inabidi ufunge madishi mengi kila dishi liwasiliane na satelaiti yake. Ndio maana ukienda katika vituo vya televisheni/ redio mfano ITV, Startimes na vingine unakuta madishi mengi ya kupokea mawasiliano (chaneli) mbalimbail toka katika satelaiti tofauti tofauti.

Masafa ya Mawimbi ya Televisheni / Redio kwenda (uplink frequencies) katika satelaiti katika eneo letu ITU Region 1 (Afrika, Ulaya, Uarabuni na Urusi)
 


Masafa yanayotumika kupeleka mawimbi katika satelaiti toka vituo vya Televisheni/Redio vinavyotumia Ku Band katika ukanda wetu (ITU Region 1) ni kati ya 14.0GHz - 14.5GHz.

Masafa yanayotumika kupeleka mawimbi katika satelaiti toka vituo vya Televisheni/Redio vinavyotumia C Band katika ukanda wetu (ITU Region 1) ni kati ya 5.850GHz - 6.425GHz.
 
CREDITS: Lukaza Blog 

       

NJIA 5 ZA UTUNZAJI WA NGOZI YENYE AFYA BORA.

 



Wanawake wengi hupenda kuwa na mvuto katika ngozi yao, hasa maeneo ya usoni mikononi na miguuni, basi njia hizi chache nilizoziandaa hapa kwaajili yako wewe unayependa kuwa na ngozi yenye afya, zitakufaa sana.

Kwanza safisha uso wako kwa maji na sabuni angalau kwa siku mara mbili. Osha kwa maji yenye joto, kwasababu maji ya moto hufungua vijitundu vilivyoko kwenye ngozi na maji ya baridi hufunga vijitundu hivyo vya ngozi, hivyo ni vyema ukaosha kwa kutumia maji ya joto pamoja na sabuni, kisha kabla ya kupaka makeup, pitisha maji ya baridi tena ili kuepusha ngozi kudhurika na hali ya hewa.

Hakikisha unapunguza matumizi ya vipodozi haraka iwezekanavyo, kwani huziba vijitundu vya ngozi vinavyofanya ngozi kupumua. Usipake vipodozi wakati wa kulala, labda vile ambavyo ni maalu kwaajili ya ngozi. Lakini kwa ushauri unatakiwa kuoondoa vipodozi vyoote katika ngozi yako kabla ya kulala.

Unapaswa kuweka nywele zako nyuma na usitumie mikono mitupu wakati unapaka creame usoni, tumia vifaa maalum vya kupakia vipodozi.

Kula mlo bora, kumbuka kujumuisha
matunda fresh na mboga za majani katika mlo wako. Matunda na mboga za majani huongeza vitamini A na vitamini E mwilini ambavyo ni vyanzo mojawapo vinavyoweza kuipatia ngozi yako muonekano mzuri na imara.

Kwa haya machache umeweza kuona kwa kifupi tu jinsi ya kuhifadhi ama kutunza ngozi yako ya uso ili kuipatia muonekano halisi wa ngozi yako.

 

SABABU ZA WATOTO WACHANGA KULIA LIA NA NAMNA YA KUWABEMBELEZA



Ni kawaida kwa watoto kulia. Hata watoto wanaozaliwa na afya njema kabisa wanaweza kulia kwa jumla ya wastani wa kati ya saa moja mpaka matatu kwa siku. Kwa vile watoto hawawezi kujifanyia chochote wao wenyewe zaidi ya kutegemea wazazi, walezi ama watu wengine wanaowazunguka katika kuwapatia chakula, joto, na faraja, kilio ni njia ya mtoto ya kuwasilisha moja ya mahitaji hayo.
Kama mzazi mpya, wakati mwingine inakuwa vigumu kutambua mtoto wako anahitaji nini anapolia. Mzazi anaweza kuwa na maswali kadhaa kichwani mwake, je, mtoto ana njaa, anasikia baridi, ana kiu, anaumwa ama amechoka? Katika siku za mwanzo, hali ya namna hii inawawia vigumu wazazi wengi, wasijue nini la kufanya. Hata hivyo, kwa kadiri siku zinavyopita mzazi mpya ataweza kutambua kuwa kilio cha mtoto wake kinamaanisha anahitaji nini kutokana na mfumo wake wa kulia.
Kadiri watoto wanavyokua ndivyo ambavyo hujifunza hatua mbalimbali za kuwasiliana na wazazi ama walezi wao. Wanakuwa na namna nzuri ya kuwasiliana kwa mfano kwa macho, na kutoa sauti, na hata kutabasamu ambavyo vyote kwa pamoja hupunguza haja ya kulia.
Sababu zinazofanya watoto kulia
Tuangalie sababu kadhaa zinazosababisha mtoto kulia na nini anachotakiwa mzazi ama mlezi kufanya pindi mtoto anapolia.
1. Hitaji la chakula
Njaa ni mmoja ya sababu kubwa inayowafanya watoto wengi kulia. Uwezekano wa mtoto kulia unaendana sana na umri wa mtoto. Kadiri jinsi mtoto alivyo mdogo zaidi ndivyo uwezekano wa kulia sana pindi anapohisi njaa unavyokuwa mkubwa, isipokuwa katika siku mbili za mwanzo baada ya kuzaliwa ambapo watoto hula kwa kiasi kidogo sana. Kwa kawaida katika siku mbili za mwanzo tangu mtoto kuzaliwa, maziwa ya kujilimbikizia mapema sana yaani ‘colostrum’ huwa ni kidogo sana kwa mama walio wengi na huanza kuongezeka kuanzia siku ya tatu baada ya kujifungua. Pia tumbo la mtoto katika kipindi hiki huwa bado dogo sana na hivyo uwezo wake wa kuhifadhi maziwa anayonyonya huwa bado mdogo hali ambayo humfanya mtoto kujisikia njaa. Hivyo kama mtoto wako analia, uwezekano mkubwa ni kuwa ana njaa na hivyo mzazi unashauriwa kumnyonyesha. Inawezekana mtoto asiache kulia mara moja, lakini mama unashauriwa kuendelea kumnyonyesha taratibu na mtoto anaweza kuacha kulia kwa kadiri anavyoburudika na chakula na kuanza kushiba. Iwapo mama unadhani mtoto wako ameshiba lakini bado anaendelea kulia, inawezekana kuna sababu nyingine zaidi.
2. Hitaji la starehe
Baadhi ya watoto wanakuwa na hisia kali pindi vitu kama nguo inapoelekea kumbana sana au iwapo anahisi kuna kitu chochote ndani ya nguo yake kinachomsababishia maumivu. Wapo baadhi ya watoto ambao hawaoneshi kuhangaika pale nepi zinapokuwa zimelowa sababu ya mkojo au kinyesi, kwa vile baadhi yao huihisi joto na hivyo kupendezewa na hali hiyo, wakati watoto wengine hulia na kuhitaji kubadilishwa nguo walizovaa mara moja, hasa kama ngozi zao laini zinasumbuliwa. Ni vyema kwa mzazi ama mlezi kumchunguza mtoto wako kama amechafua nepi na kumbadilisha. Vilevile ni vyema kuangalia kama nguo alizovikwa hazibani na hakuna chochote ndani ya nguo kinachomletea maumivu.
3. Hitaji la kuwa na joto la wastani
Baadhi ya watoto hawapendi kubadilishwa nepi au kuogeshwa. Hawajazoea kuhisi hewa yenye joto tofauti juu ya ngozi zao. Wengi wao hupendelea sana kuwa na hali ya jotojoto lililohifadhiwa. Kwa hiyo ni vyema kumbadilisha mtoto nepi haraka ili kuweza hifadhi joto lake. Inashauriwa pia kutokumvalisha nguo nyingi zaidi ya mahitaji ili mtoto asije akahisi joto zaidi ya analolihitaji mwilini na hivyo kupelekea kuanza kulia.
Inashauriwa pia kutomfunika mtoto kwa mashuka au mablanketi mengi hasa wakati wa kumlaza. Kabla ya kuamua ni kiasi gani cha nguo unachohitaji kumfunika mtoto wakati wa kulala, ni vyema kuangalia kama mwili wa mtoto ni wa moto au baridi isivyo kawaida. Unaweza kufanya hivi kwa kuhisi joto la tumbo lake kwa kutumia kiganja chako. Iwapo mtoto ana joto sana, unashauriwa kupunguza idadi ya nguo za kumfunika vivyo hivyo iwapo unahisi mtoto ana baridi isivyo kawaida inashauriwa kuongeza idadi ya nguo za kumfunikia. Usipime joto la mwili wa mtoto kwa kutumia joto la mikono au miguu yake kwani si kitu cha uhakika na mara nyingi huleta matokeo yasiyo sahihi kwa vile ni kawaida ya mikono au miguu ya watoto kuwa ya baridi.
4. Hitaji la kushikwa ama kubebwa
Baadhi ya watoto wanahitaji kuwa karibu na wazazi wao kwa kubebwa na kubembelezwa. Watoto wakubwa wanapata faraja kwa kuwaona wazazi wao wakiwa karibu na kusikia sauti zao, lakini mara nyingi watoto wachanga wanahitaji kushikiliwa na kubembelezwa kwa faraja. Kama umemlisha mtoto wako na kumbadilisha nepi wakati mwingine mtoto anahitaji kubebwa pia.
Baadhi ya wazazi uhofia kuwa wanaweza kuwaharibu watoto wao kimakuzi pindi wanapowabeba sana. Hiyo si kweli hususani kwa miezi michache ya mwanzo tangu kuzaliwa kwa mtoto. Wakati baadhi ya watoto hawapendi kubebwa, wapo wengine ambao hutaka kubebwa karibu muda mwingi. Iwapo mtoto wako ni wa namna hiyo, unaweza kumbeba mgongoni au kwa jinsi yeyote ile ambayo itakuruhusu kuendelea na shughuli zako nyingine.
5. Hitaji la mapumziko
Ni rahisi kudhani kuwa mtoto atapata usingizi wakati wowote popote pale alipo. Hata hivyo, kwa baadhi ya watoto, hali kama za ujio wa wageni, kelele au hali ya fujo zinaweza kumfanya mtoto kusisimka na hivyo kuwa vigumu kwake kutulia. Watoto wachanga wanaweza kupata ugumu wa kukabiliana na mambo ya kusisimua sana kwa mfano vitu kama taa, kelele, au kubebwa kwa kupokezana kutoka kwa ndugu au mgeni mmoja mpaka mwingine hasa wanapokuja kumtembelea mama. Hali hii humfanya mtoto kushindwa kustahamili na hivyo kuzidiwa na hayo yote. Wazazi wengi wamegundua kwamba watoto wao hulia zaidi kuliko kawaida wakati ndugu au jamaa wakiwatembelea hususani nyakati za jioni. Kama hakuna sababu nyingine maalum inayopelekea mtoto wako kulia, yawezekana basi kilio chake kinasababishwa na uchovu. Mzazi ama mlezi anashauriwa kumpeleka mtoto sehemu tulivu iwe chumbani au sehemu nyingine ambapo patamwondolea hali ya kusisimuliwa na hivyo kumfanya aweze kuacha kulia na kupata usingizi.
6. Hitaji la kitu cha kumfanya mtoto ajisikie vizuri
Iwapo umemlisha mtoto wako na kuhakikisha kuwa yupo vizuri lakini akawa bado anaendelea kulia, mzazi ama mlezi unaweza kuwa na hofu kuwa mtoto ni mgonjwa au ana maumivu. Ni vigumu sana nyakati za mwanzo kwa mzazi kutambua kuwa mtoto wake analia kwa sababu ya kutokuwa na furaha au kuna kitu kinachomuumiza. Mtoto ambaye ni mgonjwa mara nyingi hutoa sauti ya kilio kilicho tofauti na sauti yake ya kawaida. Sauti hii inaweza kuwa ya haraka zaidi au kali sana. Vile vile kwa mtoto ambaye amezoea kulia mara kwa mara, pindi anapoonesha hali ya utulivu isiyo ya kawaida inaweza kuwa dalili ya kwamba ni mgonjwa. Jambo muhimu la kukumbuka ni kwamba hakuna mtu anayemjua mtoto wako vizuri zaidi kuliko wewe. Kwa hiyo basi kama mzazi ama mlezi unahisi kwamba kuna kitu tofauti kwa mtoto wako ni vyema ukaonana na wataalimu wa afya. Wataalamu wa afya daima watayachunguza matatizo ya mtoto wako kwa umakini mkubwa na hivyo kujua sababu ya mtoto kulia. Mzazi ama mlezi unashauriwa kuonana na daktari iwapo mtoto wako ana shida ya kupumua pindi anapolia, au kama kulia kwa mtoto kunaambatana na kutapika, kuharisha ama kutopata choo.
7. Mtoto anahitaji kitu, lakini hujui ni nini
Wakati mwingine unaweza kushindwa kufahamu ni nini kinachomsababishia mtoto wako kulia. Wakati mwingine watoto wanakosa furaha. Hali hii ya kukosa furaha bila sababu inaweza kudumu dakika chache au saa kadhaa ambapo mtoto huendelea tu kulia mara kwa mara. Wakati mwingine baadhi ya watoto hulia kwa muda mrefu huku wakirusha rusha miguu. Hii hali yaweza kusababishwa na maumivu ayapatayo mtoto kwenye tumbo. Kwa kitaalamu hali hii hujulikana kama colic. Huwawia vigumu sana wazazi wengi kukabiliana na mtoto ambaye ana colic. Hakuna tiba ya uchawi kwa colic, aidha ni mara chache sana hali hii inadumu kwa zaidi ya miezi mitatu. Hata hivyo ni vyema kupata ushauri wa daktari pindi unapohisi mtoto wako ana colic.
Je, nini cha kufanya mtoto anapolia?






Kuna vitu ambavyo mzazi unaweza kufanya ili kumpa faraja mtoto wako pindi anapolia. Yawezekana baadhi ya mambo yatakayoshauriwa hapa yasiwasaidie watoto wote, hivyo basi mzazi ama mlezi ni vizuri ukamjua mtoto wako na kufahamu kwa undani ni kitu gani hasa kinachoweza kusaidia kumtuliza.
1. Kumbeba mtoto
Watoto wachanga huonyesha upendeleo fulani wa hisia, kama vile walivyokuwa ndani ya tumbo, hivyo basi unaweza kujaribu kumvingirisha mtoto wako katika blanketi au nguo zozote za kumbebea kama khanga au vitenge ili kuona kama atapenda hali hiyo. Watoto wengine hawapendi kuvingirishwa kwenye blanketi na hupenda aina nyingine ya kupata faraja kama vile kubebwa. Wapo wazazi wanaopenda kumbeba mtoto kiasi cha kumfanya mtoto asikie mapigo ya moyo, kitendo ambacho humpa faraja sana mtoto.
2. Kumwimbia nyimbo au sauti za kumbembeleza
Akiwa tumboni mwa mama, mara kwa mara mtoto alikuwa akisikia mapigo ya moyo ya mama. Hali hii ndiyo sababu kubwa ya watoto wengi kupendelea kubebwa na mama zao. Hata hivyo kuna aina nyingine za sauti zinazoweza pia kusaidia kumtuliza mtoto. Mzazi ama mlezi unaweza kujaribu kuweka muziki wa taratibu au kumuimbia mtoto nyimbo za kubembeleza kwa sauti ya chini sana. Unashauriwa kutokuweka miziki ya haraka au yenye sauti kubwa kwa sababu inaweza kumwondolea hali yake ya utulivu na hivyo kumfanya ashindwe kuacha kulia.
3. Jaribu kumkanda au kumsugua taratibu (masaji)
Kumkanda kanda au kumsugua mtoto taratibu mgongoni au tumboni kunaweza kumsaidia sana kumfariji mtoto. Iwapo inaonekana mtoto anapata tabu wakati wa kubeua au kucheua, jaribu kumlisha akiwa wima zaidi na kila baada ya kumlisha mweke juu ya bega lako na kumsugua taratibu mgongoni ili kumsaidia atoe gesi kwa kubeua. Baadhi ya watoto ambao wana “colic” wakati mwingine hutulia hasa wanaposuguliwa taratibu tumboni na hii huweza kuwafanya wajisikie vizuri kwa vile huihisi kwamba angalau mzazi ama mlezi unajitahidi kufanya kitu fulani kusaidia kumwondolea shida yake.
4. Mpatie kitu cha kunyonya
Kwa baadhi ya watoto waliozaliwa, haja ya kunyonya ni kubwa sana na hivyo kumpatia chuchu safi iliyotengenezwa kwa ajili hiyo au kidole kisafi cha mama inaweza kuleta faraja kubwa kwao. Kunyonya kutamsababishia mapigo ya moyo wake kuwa katika kiwango chake cha kawaida, kupumzisha tumbo lake, na kutulia.
Ulezi wa watoto wachanga ni kitu kigumu lakini ulezi wa mtoto ambaye hulia mara kwa mara ni ngumu zaidi. Kupata msaada na kuungwa mkono wakati unapohitaji msaada ni muhimu zaidi. Mzazi hana budi kufahamu kuwa kwa jinsi siku zinavyopita, na kwa kadri mtoto anavyokua, mtoto anajifunza njia mpya ya kuwa na uwezo wa kuwasilisha mahitaji yake na hivyo ni muhimu mzazi naye kujifunza njia hizo ili kumuwezesha kumpatia mtoto mahitaji yake anayohitaji kwa haraka na wakati unaostahili.

 

Msongo wa mawazo kipindi cha ujauzito husababisha ulemavu kwa mtoto.

 


 
Ripoti ya watafiti hao inazidi kuthibitisha matokeo ya tafiti zilizopita kuwa mama mwenye msongo wa mawazo wakati wa ujauzito kutokana na mambo kama kufukuzwa au kuachishwa kazi, kutengana na mwenza wake au kufiwa ana hatari ya kuzaa mtoto mwenye ulemavu kama vile midomo sungura (cleft lip na cleft palate) au matatizo kwenye uti wa mgongo (spina bifida).
Jopo la watafiti wa kidenmark likiongozwa na Dr Dorthe Hansen walifanya uchunguzi ili kuthibiitisha ukweli na uhakika wa dhana hii.
Wakitumia rikodi za taarifa za kitabibu za kipindi cha miaka 12 kutoka 1980 mpaka 1992 kutoka masjala ya Taifa ya kitabibu, watafiti hao waliweza kuwatambua wajawazito wote waliokumbwa na matatizo makubwa ya kimaisha wakati wa ujauzito na hata miezi 16 kabla ya kupata ujauzito. Matatizo makubwa ya kimaisha yaliyochunguzwa yalikuwa kukumbwa na msiba wa ndugu au jamaa wa karibu, ndugu au jamaa wa karibu kulazwa hospitali kwa mara ya kwanza baada ya kugundulika kuwa na kansa ya aina yeyote au ndugu au jamaa wa karibu kupatwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo. Mambo haya yalichunguzwa kwa kigezo kuwa, mjamzito yeyote aliyewahi kukumbana nayo ana hatari kubwa ya kuwa katika msongo wa mawazo bila kujali tabia yake, kama ana watu wa kumfariji au uwezo wake wa kukabiliana nayo.
Jopo hilo lilichunguza maendeleo ya mimba kwa wajawazito 3,560 ambao walikumbana na matukio hayo kwa kulinganisha na wajawazito wengine 20,299 ambao hawakukumbana na hali yeyote ambayo ingewasababishia kupata msongo wa mawazo wakati waujauzito.
Matokeo ya uchunguzi wao yalionesha kuwa ulemavu na hitilafu za viungo kwa watoto waliozaliwa ulikuwa mara mbili miongoni mwa kundi la wajawazito waliokumbwa na msongo mkali wa mawazo ikilinganishwa na kundi la kinamama ambao hawakuwa na hali hiyo.
Kadhalika ilionekana kuwa wanawake waliowahi kukumbwa na hali kama hiyo katika ujauzito mbili mfululizo za nyuma walikuwa katika hatari kubwa zaidi ya kuzaa watoto wenye ulemavu wa viungo tofauti na wale waliowahi kupatwa na hali hiyo mara moja tu au wale ambao hawakupatwa kabisa.
Ilionekana pia kuwa tukio lililoongeza uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo ilikuwa ni iwapo mjamzito atafiwa na mtoto wake mwingine mkubwa wakati akiwa katika miezi mitatu ya mwanzo wa ujauzito wake huu wa sasa. Hatari ya kuzaa mtoto mlemavu iliongezeka iwapo kifo cha mtoto huyo mkubwa kingetokea bila kutarajiwa kwa mfano kwa ajali.
Watafiti wanasema kwamba, msongo mkali wa mawazo huchangia kuathiri uumbaji wa mtoto aliye tumboni kwa kusisimua uzalishaji wa homoni ya cortisone. Homoni hii husababisha ongezeko la kiwango cha sukari katika damu na upungufu wa usambazaji wa hewa safi ya oksijeni kwa mtoto, mambo ambayo husababisha kutokea kwa hitilafu katika uumbaji wa viungo vya mtoto hatimaye kusababisha ulemavu wa viungo vya mtoto.
Uwezekano mwingine ni kuwa msongo mkali wa mawazo humchochea mama mjamzito kutumia zaidi vileo vyenye alcohol na pia kula lishe duni hali ambayo huongeza madhara zaidi kwa kiumbe kilicho tumboni.
Hata hivyo Professor Peter Hepper wa Chuo Kikuu cha Queen’s cha Belfast, anasema hakushangazwa na matokeo ya utafiti huo.
Anasema kuwa, “tunafahamu msongo wa mawazo husababisha mabadiliko ya kifiziolojia katika mfumo wa mwili wa mjamzito, na hivyo hakuna sababu kwanini mabadiliko hayo yasimfikie pia mtoto aliye tumboni kupitia kondo la nyuma na kumuathiri. Matokeo haya yanazidi kuthibitisha kile tulichokuwa tukikifahamu tangu awali kuwa msongo wa mawazo wa muda mrefu kwa mwanamke una madhara makubwa kwa mendeleo ya uumbaji wa mtoto aliye tumboni na hivyo basi hakuna budi kufanyike kila njia kuwasaidia wajawazito walio katika hali hii ili waweze kujifungua watoto walio na afya njema na salama.”

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top