Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FLORA MVUNGI ANASA TENA

flora (2)
Staa wa Bongo Muvi, Flora Mvungi na ‘kibendi’ chake.
DAR ES SALAAM: Makubwa! Ikiwa mtoto wake wa pili akiwa angali na umri wa miezi 6, staa wa Bongo Muvi, Flora Mvungi tayari amenasa ‘kibendi’ kingine huku akiwaomba watu ambao wanamshangaa wamuache kama alivyo.

flora (1)
Akizungumza na gazeti hili, Flora ambaye kwa hivi sasa ana watoto wawili; Tanzanite na Africa, amewataka watu waache kumjadili kwani hakuna ambaye anamsaidia kulea na ukizingatia watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.
“Hivi jamani kwa nini watu wanapenda kufuatilia maisha ya watu? Mimi hata kama nikizaa watoto kumi hakuna ambaye ananisaidia kulea, waniache nizae maana hawanisaidii kulea, mimi na mume wangu tumepanga kuzaa kadiri tunavyoweza,” alisema Flora.
Staa huyo alizidi kufunguka kuwa, mimba aliyonayo iliingia bahati mbaya na hawezi kuitoa hata siku moja na ni bora azae, amalize na aweze kufanya vitu vingine vya maendeleo.
“Nafikiri watu wanataka nikipata ujauzito nitoe kitu ambacho siwezi kukifanya kabisa ni bora nikazaa kisha nipumzike ili niweze kuendelea na maisha mengine,” alisema Flora.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top