Msemaji
wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud, (kushoto) akitoa taarifa
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia kwake ni Kaimu
Mkurugeniz wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo.
Badra (kushoto) akiendelea kutoa ufafanuzi.
SERIKALI
kupitia wizara yake ya Nishati na Madini imesema imetengea maeneo
maalumu wachimbaji madini wadogo nchini jumla ya hekari 197,432.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Wizara ya Nishati na
Madini, Badra Masoud, amesema lengo la kutenga maeneo hayo ni
kuendeleza uchimbaji madini mdogo ili kuwanufaisha wachimbaji .
Amesema
wizara imekuwa ikitenga maeneo maalumu au tengefu kwa ajili ya
wachimbaji madini wadogo pekee ambao ni Watanzania tu , zoezi hilo
hufanywa kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka2010 kifungu cha 16
kinachompa mamlaka Waziri wa Nishati na Madini kuhakikisha anatenga eneo
lililo wazi na lenye madini kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Badra
amesema, mara tu baada ya waziri kumaliza kutenga eneo hilo kinachofuata
ni utaratibu wa kugawa hilo eneo kwa kwa kufuata taratibu za
kisheria.
Aidha
amebainisha maeneo 34 ya sehemu mbalimbali za hapa nchini yaliyotengwa
yenye ukubwa wa hekta197,432 ambayo miongoni mwa mwake ni, Mererani
Block 1-V (Manyara), Kilindi (Tanga), Maganzo (Shinyanga), Mihama
(Mwanza), Winza(Dodoma), Kalela (Kigoma) na maeneo mengine aliyoyataja.
Wakati
huohuo alisema serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imetenga
kiasi cha Dola za Marekani milioni 3.4 kwa miaka mitatu kuanzia mwaka
huu wa fedha 2015/16 kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji madini wadogo
kwa kuwapatia ruzuku ikiwa ni awamu ya tatu ili waweze kuchimba kwa
mfumo wa kisasa na kujiongezea vipato vyao pamoja na pato la taifa.
Katika
hatua nyingine alisema utaratibu wa wachimbaji wadogo kupatiwa ruzuku ni
lazima kwanza wawe na leseni ya uchimbaji, kujaza fomu za kuomba ruzuku
na kutoa ushirikiano kwa maofisa madini wa kanda na maofisa wa madini
wakazi husika eneo hilo.
Post a Comment