Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS JAKAYA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA JENGO LA MOROCCO SQUARE JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akifungua pazia kuashiria  uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
 Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC), Zakhia Meghji (kulia) na Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi, William Lukuvi wakipiga makofi kumpongeza Rais Kikwete katika siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika sanjari na hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC), Zakhia Meghji (wa pili kulia), akimkabidhi zawadi ya sherehe yake ya kuzaliwa.
 Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifungua shampeni kumpongeza Rais Kikwete katika siku yake hiyo ya kuzaliwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki wakati wa hafla hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top