Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AFANDE SELE YU HOI TAABANI

Mgombea ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini (ACT ­ Wazalendo), Seleman Msindi maarufu Afande Sele, amesema ameshindwa kuzindua kampeni zake kutokana na kukabiliwa na ukata wa fedha. Afande Sele aliyasema hayo hivi karibuni. 

“Ni kweli mimi ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya ubunge Jimbo la Morogoro Mjini, lakini hadi sasa sijafanikiwa kuzindua kampeni zangu kwa sababu ya ukata wa fedha,” alisema Sele.

 Alisema licha ya siku kuendelea kuyoyoma, ana imani kuwa atafanikiwa kuzindua kampeni zake kabla ya Oktoba 25. “Kwa upande wa chama changu hapa Morogoro wananitegemea mimi, hata katika kuwanadi madiwani, lakini tutapambana na tutafanikiwa,” alisema Afande Sele. 

Hata hivyo, mgombea huyo alisema anaendelea na kampeni zake zisizo rasmi kwa kukutana na watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea kila kata kwa ajili ya kunadi sera za chama chake, mgombea urais wa ACT ­ Wazalendo, Anna Mghwira na madiwani wao wanaogombea kata za jimboni humo.

 “Japokuwa sijabahatika kuzindua kampeni zangu lakini nimekuwa nikijaribu kutembelea makundi mbalimbali ya watu vijiweni na kwenda kila kata kumwaga sera zangu ambazo zinaonekana kuungwa mkono na Wanamorogoro wengi,” alisema Sele.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top