Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tundu Lissu: Dr Slaa ni Muongo watanzaia Mpuuzeni.....Kinachomsumbua ni tamaa ya Urais. Tunamtaka Arudishe mali zote za Chama

 


Katibu Mkuu wa  Chadema, Dk Wilbroad Slaa, jana  alitangaza rasmi kuachana na siasa  baada  ya  kutofautiana  na  chama  chake  katika  kumpokea  Edward  Lowassa  na  hatimaye  kumfanya  mgombea  urais  wa  chama  hicho  chini  ya  mwamvuli  wa  UKAWA.

Dr. Slaa  alitoa  uamuzi  huo  jana  mbele  ya  waandishi  wa  habari  ambapo  pia  mbali  na  kutangaza  kuachana  na  siasa  aliwatuhumu  Lowassa  na  Sumaye  kuwa  ni  MAFISADI  wa  kutupwa  na  kwamba  hawastahili  kupewa  nchi .

Akijibu tuhuma za Dk. Slaa mwansheria wa CHADEMA Tundu Lissu amesema anashangaa kwamba Dr. Slaa anadai hakubaliani na uteuzi wa Lowassa kwa ajili ya kiti cha rais wakati yeye ndiye aliyepanga na kumleta Lowassa katika chama hicho.
Lissu  amesema  kinachomsumbua  Slaa  ni  tamaa  ya  Urais  maana  CHADEMA  walikuwa  wamekwisha  mteua  kugombea  urais  tangu  mwezi  mwezi  wa  kwanza.
"Kamati  kuu  ilimteua  kugombea  urais  kwa  tiketi  ya  chadema  tangu  mwezi  january  na  ilipofika  mwezi  April  kamati  ilimthibitisha  tena  kuwa  yeye  ndo  mgombea  wetu.

"Ilipofika  mwezi  wa  tano, Dr.  Slaa  mwenyewe  akaanzisha  mazungumzo  ya  kumleta  Lowassa  Chadema.

"Amesema  mshenga  ni  Gwajima,hajasema  mposaji  ni  nani.  Nani  aliyemfuata  Gwajima  kumwambia  tunamtaka  Lowassa, ni  Dr. Slaa mwenyewe.

"Yeye  ndiye  aliyemwambia  Gwajima halafu  ndo  akamwambia  Mwenyekiti  wa  chama  kuwa  Lowassa  akikatwa  tumchukue, na  tumchukue  kwa  sababu  ana  nguvu  kubwa  na  ataipasua  CCM  katikati.   

"Mbowe  alipoambiwa  hivyo  alikubali  na  Dr. Slaa  ndiye  aliyeunda  timu  ya  majadiliano  ya  Chadema  yenye  wajumbe  watatu  ambao  ni  Benson Kigaila, John Mrema, Reginald Munishi.

"Walikaaa  na  kufanya  mazungumzo  ya  kina  na  Dr. Slaa  alishiriki  kila  hatua.Majadiliano  hayo  yalikamilika  tarehe  22.7.2015  ambapo  Slaa  aliitisha  kikao  cha  kamati  kuu  cha  dharura  chenye  ajenda  moja  tu  ya  kumkaribisha  Lowassa  ili  awe  mgombea  urais  wa  Chadema."  Amesema  Lissu

Kwa nini  Dr. Slaa amewasaliti?
Tundu  Lissu  amesema  kilichomfanya  Dr. Slaa  awageuke  ni  First  Lady, kwa  maana  ya  mke  wake  ambaye  hakukubaliana  na  kitendo  cha  Slaa  kumpisha  Lowassa

Lissu  amedai  kuwa wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 July kwenye Kamati Kuu, Dr.Slaa hakulala nyumbani,  aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia mabegi nje na DR. alilala kwenye gari.

"Aliporudi  nyumbani, Slaa  alitupiwa  mabegi  nje, akalaa  kwenye  gari. Kesho  yake  akaja  na  kusema  anataka  kujiuzulu."  Amesema  Lissu  na  kuongeza:

"Slaa  anasema  hana  chama  na  hajihusishi  na  chama  chochote, lakini  cha  ajabu  ni  kwamba  mwezi  huu  amepokea  mshahara  wa  katibu  mkuu  wa  chama, bado  anatembea  na  gari  ya  katibu  mkuu  wa  chama.

"Japokuwa  amekitukana  chama, lakini  bado  anatembea  na  magari  ya  chama, nyumba  anayokaa  alinunuliwa  na  chama  na  inalindwa  na  walinzi  wa  chama.

".....Ajitokeze  atuambie  ni  nani  aliyemwandalia  huu  mkutano  wa  serena  hoteli?  hizo  gharama  zimelipwa  na  nani?  na  kwa  nini  ametamka  leo?

"....Kwa  kuwa  Slaa  amekitukana  chama,  litakuwa  ni  jambo  la  busara  sana  kama atarudisha  mali  zote  za  chama."

Akizungumzia  tuhuma  zilizotolewa  na  Dr.Slaa  dhidi  ya  Lowasaa, Lissu  amesema  CHADEMA  walimhoji  Lowassa  kuhusu  sakata  la  Richmond  na  aliwaambia  kuwa  aliyeruhusu  mkataba  wa  Richmond  uendelee  ni  Rais  Kikwete.

Nimeweka  Audio  ya  Lissu  Akiongea  hapo  chini.Bofya  play  umsikilize.
M
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top