Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAPYA TOKA JESHI LA POLISI



Ningependa kutoa tahadhari hasa kwa Wastaafu au wanaotarajia kustaafu, Idara, Wizara zote zinazoshughulika na wastaafu, Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri kujihadhari na watu wanaowapigia simu na kujitambulisha kuwa wao ni watumishi wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii na Idara zingine za Serikali na kwamba wanashughulika na mafao ya wastaafu.
Ninatoa tahadhari hiyo kwa sababu kwa kushirikiana na LAPF tumefanikiwa kumkamata mtu mmoja kwa jina la DAVID MAGESA MAKALI @ PETER MABULA na kumfikisha Mahakamani baada ya kujifanya ni mtumishi wa TAMISEMI, LAPF, PSPF na OFISI YA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA na kufanikiwa kuwaibiwa fedha kwa njia ya mtandao wastaafu kutoka katika mikoa mbalimbali.
Wanachofanya watu hao wanapiga simu Idara mbalimbali na kujifanya wapo TAMISEMI au Wizara nyingine na kuwataka wawatumie orodha ya wastaafu wa mwaka fulani pamoja na namba zao za simu. Inaonyeha kwa njia hiyo wameweza kupata orodha ya wastaafu takriban kutoka katika Mikoa 15 hususan kutoka Idara ya afya. Wakishapata orodha ya majina ya wastaafu na namba zao za simu humpigia mstaafu na kujitambulisha anatokea Wizarani na anashughulikia wastaafu ambao inaonekana walipunjwa kwenye mafao yao na inaonyesha naye amepunjwa kiasi cha milioni fulani. Ili aweze kumsaidia kurekebisha kumbukumbu na kumwezesha kupata fedha hizo amtumie kiasi fulani cha fedha. Mstaafu huyo akishamtumia hapatikani tena kwenye hiyo namba aliyotumia na mstaafu huyo anakuwa ameishaibiwa fedha zake.
Natoa tahadhari kwa wastaafu wasikubaliane na watu wa aina hiyo na idara mbalimbali zichukue tahadhari kubwa na kila mara wahakikishe kinachohitajika kinatoka katika idara husika na kwa mtu sahihi.
Pia nichukue fursa hii kutoa tahadhari kwa Vyama vya Siasa, wafuasi wao na wananchi wa Mkoa wa Dodoma kwa ujumla katika kipindi hiki cha Kampeni na baadaye kupiga kura, kutangaza matokeo na kuapisha waliochaguliwa kila mmoja azingatie utii wa sheria.
Ninatoa wito huo kwa sababu kuna baadhi ya Vyama wameishaanza kukiuka sheria kwa kuwatumia watoto na kuvuruga mikutano ya vyama vingine. Mfano tarehe 29.08.2015 huko katika kijiji cha Tubugwe Kibaoni Kata ya Chamkoroma Wilaya ya Kongwa Chama cha CCM kilikuwa kifanye Mkutano asubuhi ambao ulikuwa halali kulingana na ratiba.  Ulishindikana kufanyika baada ya vijana na watoto wadogo wakiwa na bendera za Chadema kuanza kuzunguka eneo hilo huku wakiimba. Kama hilo halitoshi walizuia barabara ili wagombea na wafuasi wa CCM wasipite. Tukio hilo bado ufuatiliaji wa kuwakamata waliohamasisha watoto hao na kushiriki katika uvunjaji huo wa sheria unaendelea.
Nichukue fursa hii pia kupiga marufuku Vyama vya Siasa vinavyotumia au wanampango wa kutumia vikundi vyenye muelekeo wa kijeshi mfano  Blue Guard, Red Briged, Green Guard n.k. kwani kazi ya ulinzi Mkoani Dodoma ni ya Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya dola.
Nitoe rai kwa kila mmoja afuate Sheria Mama Katiba, Sheria ya Vyama vya Siasa, Uchaguzi na nyinginezo zinazotuongoza katika kipindi cha Kampeni hadi Uchaguzi ili kuepuka kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
  
Imetolea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi - Misime D.A (SACP)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top