Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAGUFULI AFUNGA KAZI MKOANI MTWARA



 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli,akiwahutubia wananchi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye mkutano wa kampeni unaoendelea jioni hii katika uwanja wa Mashujaa. 

Dkt John Magufuli amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu mwaka huu ,Serikali yake itashusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa bati na saruji,amesema kuwa serikali yake inataka kurahisisha maisha ya watanzania wote na hivyo atapunguza bei ya saruji na bati na hilo litafanikiwa kwa kupunguza ushuru wa vifaa hivyo. 
"Serikali ya Magufuli nataka iwe ya kurahisisha maisha ya wananchi wake.Moja ya mambo ambayo ninedhamiria kuyafanya ni kupunguza bei ya bati na saruji.Nataka kuona watu wanajenga nyumba nzuri na za kisasa, hivyo lazima tushushe bei ya vifaa vya ujenzi,alisema Dk.Magufuli.

Alisema anatambua kiu ya watanzania ni kutaka mabadiliko ya maendeleo na kwamba Serikali yake itasimamia kuleta maendeleo ya wananchi na kazi hiyo anaiweza na ndio maana anaomba urais. " Ndugu zangu watanzania serikali ya Magufuli inakuja kuendelea pale ambapo awamu nyingine zimeishia.Tumetoka mbali ,tupo mbali na tunakwenda mbali.Nataka tuwe na maendeleo makubwa na hilo serikali yangu ndio kazi itakayofanya,"alisema Dk.Magufuli huku wananchu wakimshangilia kwa mayowe.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli,akiwahutubia wananchi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye mkutano wa kampeni unaoendelea jioni hii katika uwanja wa Mashujaa.
Wakazi wa mji wa Mtwara wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM,unaofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa CCM,wakimsikiliza mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtwara mjini,Murji Hasnein Mohamed akiwasalimia maelfu ya wananchi wa mji wa Mtwara waliofurika kwenye uwanja wa Mashujaa katika mkutano wa kampeni za CCM,jioni ya leo ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia wananchi hao .
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akijiachia jukwaani pamoja na wasanii wa kundi la Yamoto Band kwenye uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara,ambapo Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao waliofurika kwa wingi.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akijiachia jukwaani pamoja na wasanii wa kundi la Yamoto Band kwenye uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara,ambapo Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao waliofurika kwa wingi.
 Wakazi wa mji wa Mtwara ambao wamejitokeza kwa wingi hivi sasa ndani ya uwanja wa Mashujaa, mjini Mtwara kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM,Dkt John Magufuli
 Wananchi wakiwa wamekusanyika ndani ya uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara hivi sasa,kumsikiliza Dkt John Pombe Magufuli
  Wananchi wakiwa wamekusanyika ndani ya uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara hivi sasa,kumsikiliza Dkt John Pombe Magufuli.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kimya,Ali Kiba akiimba mbele ya maelfu ya wananchi wa Mtwara jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni wa CCM,ambapo Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kuwahutubia.
PICHA NA MICHUZI JR-MTWARA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top