Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Neno Fupi: Wasadikika Hawajapata Kuwa Wakweli Kwa Nchi Yao..


Ndugu zangu,
Wasadikika wako katikati ya msimu wao wa Ngoma Kuu. Katika hali ya kustaajabisha, mara hii Wasadikika wameamua kuwa kila mtu acheze ngoma atakavyo, na aimbe atakavyo. Mdundo ajichagulie mwenyewe na wimbo pia.

Jambo moja ni ukweli, kuwa Wasadikika hawajapata kuwa wakweli kwa nchi yao waliyozaliwa.
Ni kwa vile Wasadikika hawapendi kuujua ukweli wao. Wasadikika wanaongoza duniani kwa kuwa wanafiki kwa nchi yao waliyozaliwa.
Wasadikika ni mahodari sana wa kuukimbia ukweli. Kuvikimbia vivuli vyao.
Hakuna namna yeyote itakayowasaidia Wasadikika kufanikiwa kusonga mbele kimaendeleo, bali ni kwa kutambua, kuwa huu ni wakati wa wao kuwa wakweli kwa nchi yao waliyozaliwa.
Na hakuna wa kuwasaidia kuujua ukweli wao, bali ni wao wenyewe, kwenye nchi yao ya Kusadikika.
Ni Neno Fupi La Usiku.
Maggid,
Dar Es Salaam.
Mji Mashuhuri kwenye Nchi Ya Wasadikika.(P.T)

credit: Mjengwa blog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top