Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHILE MABINGWA WAPYA COPA AMERICA


Penati ya Alexis Sanchez imewapa Chile ubingwa wa Copa America kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa fainali kali na ya kusisimua iliyopigwa usiku wa Jumamosi kati ya wenyeji Chile dhidi ya Argentina na Chile kunyakuwa kombe hilo kwa penati 4-1. 
Ilibidi mikwaju ya penati iamue nani atanyanyua ndoo hiyo baada ya kushuhudia dakika 90 za mtanange huo zikimalizika bila timu yoyote kuzifumania nyavu za mpinzani wake. Zikaongezwa dakika 30 ambazo pia zilimalizika bila kumpata mbabe wa pambano hilo ndipo mikwaju ya penati ilipotumika kuamua nani ataondoka na mwali huyo aliyekuwa akigombewa na Mataifa ya 12 ya America Kusini.
Mchezo ulikuwa ni mkali na wa kasi, timu zote zilijitahidi kutengeneza nafasi na kufanya mashambulizi kadhaa lakini milango yote miwili ilikuwa migumu kuruhusu nyavu kutikiswa na washambuliaji wa timu zote mbili. 
Kombe hilo linawafanya Chile wamalize ukame wa mataji nchini kwao hasa kwenye mchezo wa soka kwasababu walikuwa hawajawahi kutwaa taji lolote kubwa la kimataifa. 
Mchezaji nyota wa FC Barcelona Lionel Messi, ameshindwa kutwaa taji kwa mara nyingine kwenye fainali yake ya pili akiwa na Argentina baada ya mwaka jana (2014) kulikosa kombe la dunia mbele ya Ujerumani kwenye fainali za kombe hilo ilizofanyika nchini Brazil. 
Messi ameshashinda mataji yote kwenye ngazi klabu, lakini ameshindwa kutwaa taji lolote akiwa ametinga uzi wa Argentina. 
Matias Fernandez, Arturo Vidal, Charles Arangui na Alexis walifunga mikwaju yao ya penati wakati wachezaji waliokosa penati kwa upande wa Argentina ni Gonzalo Higuain ambaye alipaisha juu wakati golikipa wa Chile Claudio Bravo alipangua mkwaju wa penati uliopigwa na Ever Banega huku Messi akiwa ni mchezaji pekee aliyefunga penati ya Argentina. 
-via Baraka Mpenja!
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top