Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWINGINE AFARIKI DUNIA! WALIOFUNGIWA NDANI MIAKA 10..


Mwili wa Muhadia Juma ukizikwa. Muhadia alichukuliwa kijijini kwao na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mafia kwa matibabu na mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Nassoro Hamid aliyepata taarifa za kufungiwa ndani kwa miaka kumi na mama yao kupitia gazeti hili toleo la Machi 31, mwaka huu lililokuwa na kichwa cha habari ‘MAMA AWAFUNGIA NDANI WANAYE 3 KWA MIAKA 10.’ BINTI Muhadia Juma ambaye alikuwa mmoja wa watoto watatu waliofungiwa ndani ya nyumba kwa miaka kumi na mama yao mzazi, Mwasiti Ally katika Kijiji cha Kanga, wilayani Mafia amefariki dunia Aprili 15, mwaka huu.Huyu ni kijana wa pili kufariki dunia baada ya Ally Juma kuaga dunia hivi karibuni na kufanya aliyebaki hai kuwa mmoja, Mzee Juma. Habari kutoka Mafia zinasema Muhadia baada ya kufikishwa hospitalini, alianza kupatiwa matibabu na lishe bora lakini siku hiyo ya kifo chake (Aprili 15) hali yake ilibadilika ghafla na kuaga dunia saa 1.30 usiku.Marehemu huyo alizikwa Aprili 16, mwaka huu katika Kijiji cha Kanga kilichopo kilomita 40 kutoka Mafia mjini ambapo gharama zote za mazishi ziligharamiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya.
Muhadia Juma enzi za uhai wake. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu juzi, Mkuu wa Wilaya, Dk.Hamid alisema amesikitishwa na vifo vya ndugu hao wawili waliokufa kwa mateso makubwa na ya muda mrefu.“Ni bahati mbaya sana ofisi yangu ilipata taarifa juu ya wagonjwa hao wakiwa katika hali mbaya. Nitoe wito kwa wananchi kwamba wanapokuwa na matatizo kama hayo wasifiche, watoe taarifa serikalini ili washughulikiwe mapema,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top