Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAMA AMFANYI UNYAMA MKUBWA MWANAE WA KUMZAA


Mtoto David akiwa na majeraha mwilini aliyosababishiwa na mama yake mzazi.
Akizungumza na Amani, mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema ni mara yake ya kwanza kushuhudia mama akimtesa mtoto wake wa kumzaa kama anavyofanya mama huyo.“Tunaomba vyombo vya haki za binadamu hata Jeshi la Polisi kushughulikia tukio hili haraka iwezekanavyo vinginevyo mtoto huyo ataathirika kisaikolojia, halafu cha kushangaza, ana watoto watatu, lakini ni huyu tu ndiye anayekutana na kipigo,” alisema jirani huyo.

Alisema katika kumsaidia kijana huyo, wamewahi kwenda kituo cha polisi Gongo la Mboto, lakini polisi jamii walipokwenda nyumbani hapo, waliambulia matusi.Mtoto David aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli mama yake anamtesa kwa muda mrefu na kwamba hivi karibuni alikwenda kumshtaki katika kanisa lao liitwalo Universal Ufalme wa Mungu, Mzambarauni, Ilala, Dar na alipotakiwa kumwita mama yake alikataa kwenda.
David akiwa nyumbani kwao.
“Baada ya mama kupata wito ule hata kanisani ameacha kwenda kwa kuhofia kikao na ushauri wa viongozi wa kanisa. Sina cha kufanya wala pa kwenda, namuomba Mungu anisaidie nimalize shule,” alisema kijana huyo.
Kuhusu sababu za kuteswa, alisema hafahamu chochote, ingawa alihisi huenda ni kwa sababu ya baba yake kutopeleka hela ya matumizi nyumbani, kitu ambacho hata hivyo haifahamu kwani hamfahamu mzazi wake, zaidi ya kusikia kuwa ni dereva wa daladala.
Katika hali ya kushangaza, mama huyo alipotafutwa na gazeti hili, alijibu kijeuri;
“Yule ni mwanangu, naweza kumfanya lolote lile. Mimi ni mzazi wake, natakiwa kumrekebisha kwa njia yoyote.” Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto umesema unashukuru kwa kupata taarifa hizo, kwani watahakikisha wanafuatilia jambo hilo na kulipatia ufumbuzi.
Kamanda Msangi: “Ni kweli tukio hilo limetokea na inadaiwa kuwa chanzo cha kifo cha mtu huyo ni kipigo kilichotokana na imani za kishirikina.” >>video: The dramatic moment passenger who yelled 'Jihad! Jihad!' is pinned to t
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top