Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYA YA HAI MKOANI KILIMANJARO




Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipokelewa na Mkuu mpya wa Wilaya ya Hai,Mh.Anthony Mtaka,mara baada ya kuwasili na kupokelewa wilaya ya Hai tayari kwa kuanza ziara ya wilayani humo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kuchimba msingi katika shule ya msingi Modio-Masama Mashariki,Kinana alikagua na kujionea ujenzi mpya wa shule hiyo msingi Modio iliyopata janga la tetemeko na kubomoka.
katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipita kwenye moja ya daraja maarufu sana wilayani Hai,Dara la MNEPO lililopo katika kitongoji cha Kiyungi kijiji cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
ujenzi wa daraja jipya la MNEPO ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika ukiendelea
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua ujenzi wa daraja jipya la MNEPO ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika,lililopo katika kitongoji cha Kiyungi kijiji cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani Hai,mara baada ya kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi.
Baadhi ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani Hai,wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa staili ya aina yake,alipokuwa akiondoka kijijini hapo mara baada ya kuzungumza nao kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi. SOMA HAPA KUHUSIANA NA MGOGORO HUO
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa kukagua chumba kipya cha mionzi,pichani nyuma ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh.Leonidas Gama.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifanya majaribio ya uchunguzi juu ya mkono wake kupitia mashine mpya mionzi,iliyowekwa katika chumba hicho cha mionzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Hai,mara baada ya kukagua chumba kipya cha Mionzi (X-Ray).
Baadhi ya Wakazi wa mji wa Bomang'ombe wakishangilia jambo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa mji wa Bomang'ombe jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Snow View mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Bomang'ombe jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Snow View wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
Wananchi wa Bomang'ombe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Hai,kabla ya kukagua chumba kipya cha Mionzi (X-Ray).
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top