Takribani
watu 18 wamenusurika kufa jana baada ya gari la abiria lenye T 349 CXB Kampuni
ya Sharoni liliokuwa linatokea Arusha kulekea dodoma kuanguka katika eneo la
kisongo uwanja wa Ndege Jijini Arusha.
Kwa
mujibu wa abiria walikuwa ndani ya basi hilo wamesema kuwa ali hiyo imetokea
baada ya dereva wa basi hilo kutaka kupita gari lililokuwa mbele yake bila
kuchukua tahadhari na ndipo gari hilo lilipo acha njia kupinduka.
Kwa
upande wa abiria wa basi hilo aliteyejitambulisha kwa moja la Mama Latifa
amesema gari hilo lilipoteza muelekeo kuwa mara baada ya gari hilo kufeli breki
za nyuma.
Aidha
majeruhi watukio hilo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya Rufaa
Maunt Meru Jijini Arusha na wengine wameendelea na safari huku jeshi la polisi
linaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo iliyotokea majira ya saa moja na nusu
jana asubuhi.
Post a Comment