“Rais lazima aagize vyombo vya uchunguzi kufanya
kazi yake na baada ya hapo ndipo atapata mahali pa kuanzia. Watu wengi
walitaka Rais Kikwete achukue hatua baada ya kupewa maazimio ya Bunge.
Jambo hilo haliwezekani,” Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
alisema jana na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa watakaobainika
kuwa na makosa ya kimaadili au jinai baada ya uchunguzi.
Alisema uchunguzi kuhusu uchotwaji wa mabilioni
hayo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pia
utazingatiwa na Rais katika kutoa uamuzi.
“Maazimio ya Bunge ni mazuri ila inatakiwa muda
kwanza ili Rais naye apate taarifa za uchunguzi zaidi. Maazimio hayo ni
muhimu na si ya kupuuzwa hata kidogo,” alisema.
Alisema
vyombo vinavyofanya uchunguzi kuhusu suala hilo ni vile ambavyo
vilitajwa kufanya hivyo katika maazimio manane ya Bunge.Kwa Habari Zaidi
Bofya na Endelea.....
Post a Comment