Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bilionea wa Nigeria amzawadia Tayo $350,000 baada ya kushindwa kuzinyakua $300,000 za BBA ...davido ashare picha hiyo na kusema “we do this easy, bar dey”

Tayo
Idris (kushoto) akiwa na Tayo (kulia)


Imeripotiwa kuwa baada ya mshiriki wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Afrika, Tayo kuzikosa dola laki tatu za Biggie zilizomwendea Idris wa Tanzania Jumapili iliyopita, mshiriki huyo wa Naija amezawadiwa $350,000 sawa na zaidi ya milioni 600 kutoka kwa shabiki wake bilionea.

Bilionea huyo aitwaye Ayiri Emami ameamua kuongeza dola 50,000 juu zaidi ya ile ambayo ilitolewa na Biggie ambayo ni $300,000 kutokana na kuwa shabiki mkubwa wa Tayo.
bilionea
Bilionea Ayiri Emami



Davido Tayo
Inasemekana hii si mara ya kwanza kwa bilionea huyo kumwaga mkwanja mrefu kwa wasanii anaowapenda, aliwahi kufanya hivyo kwenye harusi ya 2Face 2010 ambapo inasemekana alitoa zaidi ya Naira milioni 20 ( sawa na zaidi ya Tsh 189,000,000) na kumzawadia Range Rover mpya, na pia alimzawadia msanii mwingine aitwaye Durella gari aina ya Toyota Prado Jeep.

Staa wa Nigeria Davido ameshare picha ya story hiyo Instagram na kuandika “we do this easy, bar dey” .
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top