Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MFAHAMU KIJANA SANDE MWENYE MIAKA 25 AKIWA NA KILO ZAIDI YA 250 ANAVYOTESEKA ,ASHINDWA KWENDA INDIA KWA MATIBABU


Kijana Sande Mrema Mwenye tatizo la uzito wa kilo 250 na umri wa maiaka 25 ameshindwa kusafiri kwenda nchini india katika matibabu yake baada ya kushushwa mara kadhaa kwenye ndege za kimataifa anazotakiwa kusafiria licha ya ndugu zake kulipa Gharama zote za usafiri wake.Akizungumza kwa Masikitiko eneo la karakana katika moja ya Hoteli anapoishi kwa sasa wakati akisubiri miujiza ya kupatikana kwa Ndege Bwana Sande Mrema aliyehitaji waandishi kumfunika uso wakati wa mahojiano amesema anateseka sana na uzito wake unazidi kuongezeka siku hadi siku lakini hajafanikiwa kusafiri.
Dada wa mgonjwa huyo anaeleza namna ambavyo wameteseka kumuhudumia ndugu yao mapaka sasa na Kuomba serikali kuingilia kati kufanyanikisha safari ya ndugu yao kwani ameshawasiliana na Daktari wake na malipo wameshafanya ila tatizo ni kupatikana kwa nafasi katika Ndege.
Licha ya ITV kujaribu kutafuta wahusika wa Ndege hizo na kushindikana kwa leo,mama mdogo wa kijana huyu anaelezea ndege walizolipia na kushindikana hivyo kuomba waziri wa afya na ustawi wa jamii,waziri wa uchukuzi na viongozi wengine kuwasaidia ili nafasi ya kusafiri kupatikana.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top