Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAPYA YAIBUKA UMRI WA MISS TZ 2014, CHETI CHAKE CHA KUZALIWA OUT...


Nakala ya Hati ya Kusafiria ya Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu ambapo inaonyesha ana miaka 25 sasa Aliyesema ana miaka 18, 23 tumueleweje?PICHA KWA HISANI YA JAMII FORUMS.
Hii ni nakala ya Leseni ya Udereva ya Miss Tz 2014 ambayo inaonyesha amezaliwa 31/5/1989 sasa hapa mbona kuna mkanganyiko yupi anasema ukweli?
Nakala ya Cheti halisi cha Kuzaliwa cha Miss Tz 2014 Sitti Mtemvu kikionyeshwa leo wakati kamati ya Miss Tz ilipokutana na wanahabari kwaajili ya Kuzungumzia swala la Umri wa Miss Tz 2014
Baada ya maneno mengi kuzungumzwa na wadau wa maswala ya Urembo Nchini na kuandikwa sana kwenye Mitandao ya Kijamii ambapo headline ilikua ni Umri wa Miss Tz 2014 leo Kamati ya Miss Tz ikiongozwa na Bosi wao Hashim Lundenga wahitisha mkutano na waandishi wa Habari kwa kwaajili ya kuzungumzia Umri sahihi wa Miss Tz 2014 na kuamua kuonyesha cheti chake cha Kuzaliwa Mbele ya Waandishi wa habari.

Mara baada ya  Kuonyeshwa kwa cheti cha Kuzaliwa cha Miss Tz 2014 mapya yaibuka ambapo watu mbalimbali nchini wamekuwa wakijiuliza je zile nayaraka zilizokuwa zikionyeshwa katika Mitandao ya Kijamii sio zake au je Walikosea?

Sasa tujiulize swali Dogo tu...Tumeona cheti ndio lakini cheti hiko sawa hatukatai kwa hilo lakini Je Zile nyaraka zilizozagaa kama hati yake ya Kusafiria ambayo imeonyesha kazaliwa Mwaka 31/05/1989 ilikosewa? Sio yake? au Mamlaka husika ambayo ni Uhamiaji Walifoji na ili iweje? Hapa ndipo inapotupa shaka kuendelea kuamini kamati ya Miss Tz kwasababu sio hati ya Kusafiria tu Je Vipi Kuhusu Leseni yake ya Udereva ya Huko Texas Nchini Marekani nayo si yake? au nayo Wamekosea?

Napata Shida kufahamu na kuelewa kwanini hili limetokea hivi  kwa Maana Umri wake Upo kwenye nyaraka Muhimu sana Ambazo naamini Kabisa Uhamiaji hawawezi kukosea kirahisi katika umri wa mtu na Vilevile leseni ya Udereva nayo Ya Huko Marekani nayo ya Magumashi au?

Kipi kieleweke hapa Maana Cheti kilichoonyeshwa leo kinaonyesha ana Miaka 23 ambapo amezaliwa 31 May 1991 na Nyaraka hizo hapo Juu Kuanzia Hati yake ya Kusafiria inaonyesha Amezaliwa tarehe 31 May 1989 sasa kipi ni kipi maana hata leseni yake ya Udereva ya Huko Marekani inaonyesha inaonyesha amezaliwa tarehe 31 May 1989 sasa hapa bado Hakijaeleweka....

Kazi Kweli Kweli.....
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top