Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS JAKAYA KIKWETE AOMBWA MSAMAHA


KATIKA machapisho ya gazeti hili la Tanzania daima, toleo namba 3554 la Agosti 27, 2014 na toleo namba 3555 la Agosti 28, 2014 tulikuwa na habari zenye vichwa: Kikwete anywea na Kikwete ‘alamba matapishi’ yake.
 
Vichwa hivyo vya habari vilileta mkanganyiko mkubwa serikalini, na Ofisi ya Msajili wa Magazeti, kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) ilitutaka tutoe maelezo, kwa msingi kuwa vichwa hivyo vya habari vilikuwa vinamdhalilisha Rais.

Tulifafanua maana halisi ya vichwa hivyo na habari zilizoandikwa lakini ufafanuzi wetu haukumridhisha , msajili na kutaka tuombe radhi tena.

Tumeona ni jambo la busara zaidi kuomba radhi kwa mara nyingine tena kwakuwa hatukukusudia kumdhalilisha Rais
Kwa kuzingatia misingi ya kitaaluma na hasa baada ya kubaini mkanganyiko uliosababishwa na ukali wa maneno ya vichwa hivyo vya habari, tumeona ni jambo la kiungwana kuomba radhi kwa mara ya pili katika ukurasa wa mbele habari husika  zilipoandikwa.

Na kwa kuwa tumegundua kwamba aliyekwazwa ni Rais mwenyewe, tumesukumwa na utu na taaluma kumwomba radhi Rais mwenyewe kupitia gazeti hili.
Habari iliyokuwa na kichwa cha habari: Kikwete anywea, haikulenga kumdhalilisha au kumshusha hadhi Rais, bali kuelezea kwamba baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu umuhimu wa yeye kukutana na viongozi wa Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA), hatimaye amelegeza msimamo, amekubali kukutana nao.
Ushahidi ni kwamba vikao hivyo vimekuwa vinaendelea kwa nyakati tofauti. Ukweli ni kwamba visingefanyika kama rais na washauri wake wasingelegeza msimamo.

Kuhusu habari iliyosema: Kikwete ‘alamba matapishi yake’, lengo lilikuwa kusisitiza jinsi Rais Kikwete alivyobadili msimamo ghafla na kutetea jambo alilowahi kupinga kwa nguvu zote.

Hii ilitokea baada ya Rais Kikwete kusema hadharani kwamba serikali yake inafikiria kutoa elimu bure, sera ambayo katika uchaguzi wa mwaka 2010 ilikuwa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), huku yeye na chama chake wakiibeza.

Tunachukua fursa hii kumuomba radhi Rais pamoja na watu wote walioguswa kwa namna moja au nyingine na vichwa vya habari vya magazeti husika.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top