Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Maslahi ya taifa yamezingatiwa katika Rasimu ya katiba ya sasa- Kingunge


Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania Kingunge Ngombale Mwiru amesema Katiba ya sasa imezingatia masuala ya Msingi na kuwa bora zaidi na kuongeza kuwa vipengele viliyoondolewa ni kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.


Akichangia rasimu iliyopendekezwa jana bungeni mjini Dodoma Kingue alisema hata kuondolewa kwa mfumo wa Serikali Tatu ni kwa kuwa muundo huo ulikua umelenga kuuvunja muungano jambo ambalo halitakua na maslahi ya Taifa.

Kingunge amesema Katiba ya sasa ni bora kwa kuwa imezungumzia utatuzi wa matatizo mbalimbali ya Wananchi na Kuongeza kuwa ili kuweza kupata heshima na kuwaenzi waasisi wa Taifa ni Kutengeneza katiba bora itakayoimarisha Muungano.

Aidha katika hatua nyingine, mjumbe wa bunge hilo, Stephen Wassira, yeye alitaka Katiba Mpya inayopendekezwa, iruhusu kila raia anaejua kusoma na kuandika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, kwa kuwa suala la kushika madaraka ni haki ya kila Mtanzania.

Wassira ambaye pia ni mbunge wa Bunda mkoani Mara, alitoa pendekezo hilo mjini Dodoma, wakati wa kuchangia rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, na kutahadharisha kuwa elimu isiwe kigezo cha kuwazuia raia haki yao ya msingi ya kushiriki katika kuiongoza nchi yao.

Wasira aliongeza kuwa mazingira ya elimu nchini yameshindwa kuwaandaa Watanzania wote kuwa na elimu ya juu na kwamba kuna idadi kubwa ya Watanzania wana uwezo wa kuongoza licha ya kuwa na kiwango kidogo cha elimu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top