Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KINANA AWA GUMZO



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwapungia mkono wakazi wa Bagamoyo wakati wakiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa shule ya Msingi Jitegemee.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi mshahiri maarufu wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Ali Pongwe baada ya kutoa ushairi mzuri kabla ya kuanza kwa mkutano.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo ambapo aliwasisitiza kujiunga na mfuko wa afya ya jamii pamoja na wazazi kuwapeleka watoto shule pia aliwashauri wazazi kuchagua watu wenye shughuli zao kuingia kwenye kamati za shule kwani kutasaidia sana kupunguza michango isiyo ya lazima.
 Wananchi wa kata ya Magomeni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni na kuwataka kuhakikisha watoto watakaochaguliwa kuingia sekondari wanaenda shule kwani kushindwa kufanya hivyo ni kurudisha nyuma maendeleo.Pia aliwataka wananchi wachunge afya zao kwani elimu ya maambukizi ya ukimwi inatolewa ya kutosha hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na afya yake.
 Sehemu ya watu waliohudhuria mkutano.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni ambapo alitoa sifa kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani kwa utendaji wake wenye ufanisi mkubwa pia aliwaambia wananchi hao kuwa vyama vya siasa ndio vimeshafika muda wake kwani havina sera na vimeshindwa kuja na sera mbadala ya kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.
 Wananchi wakimsikiliza Nape Nnauye ambaye pia aliwataka watendaji wa Serikali kuwa karibu na wananchi kwani kutasaidia kufanikisha maendeleo na kuondoa sintofahamu za wananchi wanaotaka kujua taarifa za maendeleo ya miradi au maeneo husika.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk.Shukuru Kawambwa akihutubia wakazi wa jimbo lake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Jitegemee ambapo aliwaambia kero za michango midogo midogo zinaondolewa .
 Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni ambapo aliwaambia  wanawake kutokuwa nyuma katika kuomba nafasi za uongozi katika chaguzi zinazokuja.
 Mmoja wa wananchi waliofika kwenye mkutano akiuliza swali kwa Katibu Mkuu wa CCM wakati wa mkutano .

 Diwani wa kata ya Magomeni Bi.Mwanaharusi Jarufu akijibu moja ya maswali yaliotoka kwa wananchi.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo akijibu maswali kutoka kwa wananchi
Sehemu ya wanachama wapya waliopokea kadi zao za uanachama leo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo zaidi ya wanachama 338 walijiunga na CCM.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimianana Mbunge wa Bagamoyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, wakati wa mapokezi yaliyofanyika eneo la Yombo jimboni humo wakati Kinana akitoka wilaya ya Kibaha leo, Septemba 21, 2014, akiwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Pwani.
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye akimsalimia Dk. Shukuru Kawambwa  wakati wa mapokezi ya msafara huo wa Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipiga lipu kushiriki ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati ya Kata ya Yombo, wilayani Bagamoyo mkoa wa P)wani, leo, Septemba 21,2014. Ujenzi wa zahanati hiyo umepangwa kugharimu sh. milioni 87.
Kinana akizunguza na wananchi nje ya jengo hilo la wodi ya Kinamama
Kinamama wakiselebuka kuchsakata muziki uliokuwa ukitumbuizwa na kikundi cha sanaa cha Bagamoyo, kumlaki Kinana alipowasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Bagamoyo leo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizindua Jengo la Ofisi ya Ofisa Mtendaji Kata ya Dunda wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani
Kinana na Nape wakiwa na Dk. Shukuru Kawambwa, wakienda kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bagamoyo, PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani kata ya Kilangalanga ambapo alitoa maoni yake kuhusu Muungano.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mlandizi, Jimbo la Kibaha kijijini ambapo aliwasisitiza wananchi hao kuiamini CCM kwa maendeleo yao na pia kupeleka watoto shule za sekondari na kujiandikisha kwenye mfuko wa afya ya jamii.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mamia ya wakazi wa Mlandizi kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani kata ya Kilangalanga ambapo aliwaambia wasibabaike na wapinzani kwani hawapo kwa ajili ya maslahi ya watu na maendeleo yao.
 Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Ndugu Hamoud A. Jumaa akielezea maendeleo yaliyofanyika katika miradi mbali mbali jimboni kwake.
 Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akiwasalimia wakazi wa Mlandizi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mtongani.
 Diwani wa Kata ya Kilangalanga  Fatma Shari maarufu kama Mama Kisebengo akihutubia wananchi wa kata yake wakati wa Mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya watu .
 Mradi wa maji wa Boko Mnemela unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 490 uawasaidia zaidi ya wakazi 4500.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiranda mbao baada ya kufungua shina la wakereketwa  la mafundi seremala  Tawi la Mshikamano.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimbeba mtoto Ashraf Wazir wa Mlandizi.
 Wananchi wa Shina la Wakereketwa mafundi Seremala wakiwa wamejipanga wakati wa zoezi la ufunguzi wa shina lao leo Mlandizi.

Mganga Mkuu wa Wilaya Dk. Victorina Ludovick (kulia)  akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) kwenda kwenye kituo cha afya cha Mlandizi ambap pamoja na kushiriki ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti, Katibu Mkuu alishiriki kupanda miti na kupokea taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu .


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishiriki ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya cha Mlandizi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya Baraza la Ardhi usuluhishi kata ya Mlandizi. (Picha zote na Adam Mzee)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top