Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kesi ya Emmanuel Mbasha imesogezwa tena mpaka October.


Mbasha 1 
Kesi ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha imepigwa kalenda kwa mara nyingine tena kwa sababu Hakimu anayeendesha kesi hiyo kupata shughuli nyingine nje ya ofisi.

Mbasha alipanda kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake hiyo ambapo mwendesha mashtaka Kiyoja Catherine aliahirisha kesi hiyo kutokana na Hakimu Williberforce Luwhego kupata dharura.
mbasha 2 
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena 17 October mwaka huu ambapo Mahakama itaanza kusikiliza ushahidi ambapo upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi wanne kwenye kesi hii inayomkabili mume wa Flora Mbasha anaekabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mara ya mwisho kabla ya hii kuahirishwa Flora Mbasha alikwenda Mahakamani kwa mara ya kwanza akiwa na watu wake na hakukutana wala kuongea na mume wake ambapo muda mfupi kesi hiyo ikaahirishwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top