Hivi
karibuni kumekuwa na tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikiripotiwa na
baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii kuhusiana na
kunyanyaswa, kutendewa vitendo visivyo vya kiungwana na kuteswa gerezani
kwa Watuhumiwa wa Makosa ya Ugaidi kinyume na taratibu za Uendeshaji wa
Magereza.
Kufuatia
tuhuma hizo, Jeshi la Magereza Tanzania Bara limefanya uchunguzi kwa
kufanya mazungumzo na Watuhumiwa wenyewe na wamekanusha tuhuma hizo
dhidi ya Jeshi la Magereza. Ukweli ni kuwa taarifa hizo si za kweli na
hatuelewi kusudio lao ni nini.
Jeshi
la Magereza Tanzania Bara linatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia
Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa
kuhusiana na Utunzaji wa Wahalifu na haki zao kwa kuzingatia misingi ya
Haki za Binadamu. Vitendo vya kunyanyasa au kudhalilisha Wafungwa
vinakemewa vikali magerezani na si Sera ya Jeshi la Magereza au
Serikali.
Napenda
kuufahamisha umma kuwa Mahabusu hao wanaotuhumiwa kwa Makosa ya Ugaidi
wapo salama, wana Afya nzuri na hawana tatizo lolote gerezani.
Imetolewa na;
John Casmir Minja,
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
20 Septemba, 2014.
Post a Comment