Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ANGALIA PICHA MATESO ANAYOPATA DADA

 


Kaseli James mwenye umri wa miaka 29, mkazi wa Kijiji cha Stela Kata ya Kagea Wilaya ya Chato, mkoani Geita, anapata maumivu makali mwilini mwake kufuatia uvimbe mkubwa katika mdomo wake, unaomsumbua kwa muda wa miaka minne sasa.
Bi. Kaseli James, akiwa na uvimbe mkubwa mdomo wake . Licha ya kupata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa kipindi chote hicho, lakini maumivu yake yamekuwa yakiongezeka kila siku huku wataalamu wa hapo wakishindwa kutambua tatizo hasa linalomsumbua. Akisimulia mkasa uliompata, wakati huu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kaseli anasema alijisikia vibaya baada ya kuambiwa hivyo, kwani hakuwa na fedha na wala hakujua ni nani angeweza kumsaidia. 
“Nilikata tamaa nilipoambiwa na madaktari kwamba matibabu yangu mpaka Muhimbili, niliamini ningefia kijijni kwetu, lakini Mungu alinipa nguvu nikawa napita kwa ndugu na maskini wenzangu walinichangia hadi zikafika shilingi 50,000 nilifanya nauli, wakati nakuja hata hela ya kula njiani sikuwa nayo, nilifika na kulazwa,” alisema. 
Tatizo lake lilianza mwaka 2010 alipojisikia kupata uchungu wa jino, uliofuatiwa na kuota kwa kijipele ambacho baadaye kilitumbuka kama vile ni jipu.
“Kimsingi tangu nianze kuumwa sijawahi kupata matibabu ipasavyo, tatizo sina hela, hata kule nyumbani mara nyingi nilijiuguza kienyeji tu, huku mdomo ukiendelea kuvimba na kushindwa kula vizuri,” alisema mama huyo. 
Aliongeza kuwa, wakati akiwa bado mzima, alijaaliwa kupata mtoto na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Frank Samson, lakini baada ya ujauzito baba huyo aliingia mitini na kumtelekeza bila huduma yoyote hadi hivi sasa.
Mwanamke huyo ambaye amelazwa Wodi namba 24 Jengo la Sewa Haji, anasema amefanyiwa vipimo, lakini bado tatizo lake kubwa litakuwa ni gharama za matibabu, kwani hata kaka yake aliyeongozana naye hana sehemu ya kulala wala kula.
 
Muonekano wa karibu wa uvimbe huo. “Nimekuja na kaka ili aweze kufuatilia matibabu yangu lakini ndiyo hatuna uwezo wa kipesa na wala mahali pa kulala kaka yangu, kwa kweli tupo katika wakati mgumu sana.“Huko nyumbani kwetu hatuna ndugu mwenye uwezo ambaye anaweza kutusaidia wala hatuna vitu vya thamani ambavyo tungeviuza na kupata fedha za kugharamia matibabu yangu. 
“Kwa kifupi maisha yetu ni magumu kwani kule kijijini tunategemea kilimo cha jembe la mkono, kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuna wakati tunakosa mavuno hivyo kuwa na tatizo la chakula.
“Nitoe shukrani kwa madaktari na manesi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, walionipokea vizuri na hadi muda huu nimeshapimwa vipimo mbalimbali nasubiri majibu, lakini ndiyo bado kilio changu kipo kwenye gaharama za matibabu,” alisema Kaseli.
Mama huyo anasema kuwa baada ya kuondoka wilayani Chato kwenda Muhimbili kimatibabu, mwanaye aliyemtaja kwa jina la Modesta Frank, alimuacha kwa baba yake mzazi (babu) ambaye ni mzee akiwa na hali mbaya kiuchumi hivyo haelewi wanaishije.
Kwa yeyote aliyeguswa na matatizo ya mama huyu, anaweza kuwasiliana naye kwa namba yake ya mkononi 0754 912453 au kumtembelea Wodi Namba 24, Jengo la Sewa Haji Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top