Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwanafunzi Amuua Mwanaye kwa kumnyonga na kisha kumficha uvunguni


Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Chimala wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya, Vena Mtati (27) (pichani) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa madai mazito ya kumuua mtoto wake kwa kumnyonga, kumtumbukiza kwenye mfuko wa rambo na kuutia ndani ya mfuko wa salfeti kisha kuuficha chini ya kitanda.

Tukio hilo la kikatili ambalo limewashangaza wengi, hasa ikizingatiwa kuwa mtuhumiwa huyo anajua sheria kwa sababu anajifunza uuguzi, lilijiri Agosti 21, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kijiweni, Kata ya Mvinjeni mjini hapa.
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye anaishi jirani na nyumba inayodaiwa kufanyika mauaji hayo (jina lipo), wiki mbili zilizopita, mtuhumiwa huyo alifika kwenye nyumba hiyo akitokea chuoni akiwa na ujauzito.
“Wiki mbili zilizopita, Vena alifikia kwa rafiki yake anayeitwa Joyce ambaye alikuwa amepangisha katika hiyo nyumba. Vena alikuwa na mimba kubwa, baada ya siku tano tu akajifungua,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza: “Siku ya tukio, Joyce yeye ambaye ni mwenyeji alitoka kwenda katika shughuli zake, akamuacha Vena akiwa chumbani. Nadhani ndipo aliposhikwa na uchungu, akajifugua mtoto wa kike.
“Ilikuwa asubuhi, sisi tukasikia kelele kutoka kwenye chumba hicho. Zile kelele zilikuwa si za kawaida! Ilikuwa kama vile kuna mtu anakabwa.

“Tuliposikiliza kwa makini, mara sauti ya redio ikaongezwa ili kufanya kelele hizo zisisikike kwa nje. Lakini kwa vile sisi majirani tulijua kwamba ndani ya chumba kile kuna mjamzito na kelele alizopiga mtoto si za kawaida ndipo tulipomtafuta mwandishi wa habari (hizi),”kilisema chanzo hicho.
Mwandishi wetu alipopatikana na kunyetishiwa kuhusu kuwepo kwa uwezekano wa mama ambaye ni nesi kumuua mtoto wake aliyejifungua, aliwasiliana na Polisi wa Dawati la Jinsia.
Denti (aliyeshika kiroba chenye mwili) akiwa chini ya ulinzi wa polisi (Kulia) ni mwenyeji wake, Joyce.
Polisi hao, awali walimtafuta mwenyeji wa mtuhumiwa huyo, yaani Joyce ambaye alikuwa kwenye mihangaiko yake.

Alipopatikana alipokonywa simu yake ya mkononi ili asiweze kuwasiliana na mtuhumiwa.
Aliulizwa kama ana mgeni nyumbani kwake, akakiri. Akaulizwa kama mgeni huyo amejifungua, akakataa ndipo wakamchukua kwenda naye nyumbani kwake kumfuata mtuhumiwa huyo.
Mwandishi wetu akiwa ameongozana na askari hao walifika kwenye chumba hicho na kumkuta Vena akiwa amesimama mlangoni.
Alipoulizwa kama amejifungua, awali alikataa katakata lakini baada ya kubanwa na kutishiwa kuswekwa ndani, alikiri kujifungua na kusema kwamba mtoto huyo amemficha uvunguni mwa kitanda.

Ndani ya chumba hicho, sakafuni kulikuwa na damu zilizodaiwa kumtoka mtuhumiwa huyo wakati akijifungua mwenyewe!
Polisi walizama chumbani, wakainama kuchungulia chini ya kitanda. Walichoanza kukiona ni mfuko wa salfeti, wakauvuta kuutoa. Walipofungua ndani, wakakuta mfuko wa rambo, wakaingiza mkono na kutoa kifurushi kikiwa kimeviringishwa nguo nyingi na ndiye mtoto huyo alimohifadhiwa.
Mbali na mwili wa mtoto huyo kuviringishwa nguo hizo, pia ulimwagiwa chumvi na vumbi la mkaa ambapo ilidaiwa mtuhumiwa alifanya hivyo ili mwili huo usitoe harufu utakapotupwa porini.
Majirani walisema maarifa hayo, mtuhumiwa aliyapata kwa sababu tayari anajua namna ya kuhifadhi mwili wa mwanadamu, kwa mwanamke asiye na ujuzi asingeweza kufanya hivyo.

Kuna madai kwamba, mtuhumiwa huyo aliwaambia polisi kuwa alifikia uamuzi wa kumuua mtoto huyo kufuatia mwanaume aliyempa ujauzito aishiye jijini Dar es Salaam kumuahidi ndoa lakini akaingia mitini.
Baada ya polisi kusikiliza maelezo ya mtuhumiwa huyo, walimkamata yeye, mwenyeji wake Joyce na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye jina halikupatikana mara moja.
Polisi walisema mmiliki wa nyumba hiyo alikamatwa kwa sababu alikiuka sheria za mji ambapo alitakiwa kutoa taarifa za kumpokea mgeni huyo kwenye serikali za mitaa lakini hakufanya hivyo huku Joyce akidaiwa kutambua kuwa mgeni wake alijifungua lakini akawaambia hakujifungua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Credit:Uwazi/Gpl
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top