JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
|
|||
|
|
|
|
TAARIFA KWA UMMA
WAZIRI
WA NISHATI NA MADINI PROF. SOSPETER MUHONGO KUWA MGENI RASMI SIKU YA WANATAALUMA
UJERUMANI
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo atakuwa
mgeni rasmi katika siku ya wanataaluma itakayofanyika Aprili 26, mwaka huu katika
mji wa Berlin, Ujerumani ambapo atazungumzia fursa za uwekezaji Tanzania
hususan katika sekta ya mafuta na gesi.
Profesa Muhongo
atatoa mada hiyo ya fursa za uwekezaji nchini ikiwa ni moja ya shughuli
zilizopangwa kufanyika katika siku mbili za kongamano la uwekezaji
litakalofanyika katika mji wa Berlin, nchini humo mnamo tarehe 25 na 26 Aprili
mwaka huu.
Kongamano hilo la
uwekezaji limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania
nchini Ujerumani ikiwa ni njia mojawapo ya kusheherekea Jubilee ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar ambapo makampuni mbalimbali kutoka Tanzania yanatarajia
kuonesha shughuli zinazolenga katika
kuonesha fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.
Mada nyingine
zitakazowasilishwa katika siku mbili za kongamano la Uwekezaji Ujerumani ni
pamoja na mahusiano baina ya Ujerumani na Tanzania na hatma ya majengo ya
kihistoria Tanzania.
Kongamano hilo la
siku mbili litaenda sambamba na maonesho ambapo watendaji wa Wizara na Taasisi watapata
fursa ya kuelezea fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta sekta ya Nishati na
Madini ikiwemo umeme, gesi asilia na mafuta, nishati jadidifu na kutoa maelezo
kuhusu ramani zinazoonyesha madini yanayopatikana nchini.
Imetolewa;
BADRA MASOUD
MSEMAJI WA WIZARA
22/4/2014
Post a Comment