Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MOURINHO ATHIBITISHA TERRY KUKOSA MECHI YA MARUDIANO, CECH MSIMU KWISHA!!



 JOSE Mourinho amethibitisha kuwa Peter Cech atakosa mechi zote zilizosalia msimu huu baada ya kuteguka bega, lakini amesisitiza kuwa Chelsea inahitaji kufika fainali ili John Terry apate nafasi ya kucheza tena.
Cech aligongana na Raul Garcia kipindi cha kwanza katika suluhu ya bila kufungana na Atletico Madrid na alipelekwa moja kwa moja hospitali kupimwa.
Wakati huo huo, Terry aliumia kifundo cha mguu baada ya kukanyagwa na Diego Costa katika dakika ya 71.
Nahodha huyo wa Chelsea alijitahidi kuendelea kucheza lakini alishindwa na kutoka.
“Peter Cech msimu kwake umekwisha” Mourinho amewaambia waandishi wa habari baada ya mechi.
“Kwa John (Terry), tunatakiwa kucheza fainali ili acheze tena”.
Terry na Cech watakosa mechi ngumu ya ligi kuu England dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield jumapili ya wiki hii na mechi ya marudiano na Atletico aprili 30 mwaka huu darajani.
John Obi Mikel na Frank Lampard watakosa mechi ya marudiano kufuatia kupata kadi mbili za njano, lakini Branislav Ivanovic  atakuwepo baada ya kumaliza adhabu yake ya kusimamishwa;
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top