Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MACHOZI MAZITO YA UKAWAZ HAYA HAPA KWA BIG BOSS MWIGULU NCHEMBA,WAREJEA BUNGENI


Viongozi na wafuasi wa UKAWA mamlalamikia Mwigulu Nchemba kwa kufuta posho zao.
Siku chache baada ya Naibu Waziri wa fedha kufuta malipo ya wabunge waliosusia vikao Dodoma, kundi hilo limemrushia maneno makali Mwigulu kwa Kitendo chake cha kuwafutia malipo yao. Paparazi wetu aliyekwepo kwenye hafla fupi ya kuzaliwa kwa mtoto wa Mbowe aliyezaa na mbunge wake wa Viti Maalumu Joyce Mukya walisikika wakisema "huyu jamaa dikteta sana sijui Kikwete alimtoa wapi,Waziri gani anaingilia mambo ya Fedha za Bunge?
Anawaza kimasikini kila wakati, tazama ilikuwa tulipwe laki 8 kwa siku bunge lote la
katiba, pia wenzake walipanga mwishoni watulipe milioni 5 kila mbunge kama gratuity yeye alipoteuliwa tu kikao cha kwanza akimwakilisha waziri akaifuta ile milioni 5 na akakata posho tokea laki 8 hadi upuzi huu wa kulipana laki 3 kama wanafunzi. Ametufanya tuishi maisha ya shida. Pia viongozi wenzake walishakubali kuongeza walau iwe laki 7 akakataa tena akawatolea lugha ya kidikteta mpaka wabunge wenzake wa ccm kuwa wanaona laki 3 ni ndogo waondoke"
Mwigulu alikemea wabunge waliokuwa wakidai nyongeza ya posho tokea laki tatu hadi saba na kusema Wajumbe wa Bunge la Katiba hawajakodishwa  tokea kenya au uganda au ulaya kuja kututungia katiba,Wanatunga Katiba ya Nchi yaoi wajibu wao.
Aliendelea Kusisitiza katika nukuu zake kwa Vyombo vya Habari kuwa " Mnatimiza wajibu wenu. Ninyi sio consultants wa kukodiwa. Mko sawa na mfugaji anayelisha mifugo yake, sawa na mkulima anatetunza shamba lake au muuza duka anayeuza duka lake. Anayeona hapa hapati hela anapoteza muda kwa heshima zote afungashe mizigo yake aondoke kesho"alisikika Mwigulu.
Wiki iliyopita wajumbe wa CHADEMA NA CUF kabla ya Kususia  Bunge walisaini fedha ya tar 16 hadi 30 karibu nusu mwezi huku tar 17 wakajitoa kwenye bunge hilo wakijua bunge limeshapeleka hizo hela benki,Jambo ambalo limetajipambanua kuwa ni Ukosefu wa Uzalendo na jambo la Kupanga kunufaika na Fedha za Umma kwa njia ya Wizi.
Mapema baada ya Wanaojiita UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba,Mh:Mwigulu ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha aliagiza Wajumbe wa Bunge kukusanya saini upya na kufutilia mbali malipo ya awali waliopeleka benk. Harakaharaka mwigulu akaagiza benki kurudisha cheki zote bunge zikaandikwe upya.
Mwigulu Nchemba alikwenda mbali zaidi kwa Kusema,Kupitia Mwenyekiti wa Bunge,Rais atengue Uteuzi wa Wajumbe waliosusia Bunge la Katiba,Pia kwa Wale Watumishi wa Serikali waliokuwa Wajumbe wa Bunge la Katiba na hatimaye Kujitoa na UKAWA Waangaliwe Utumishi wao na Ikiwezekana Serikali itoe adhabu stahiki kwa Walengwa mbali na kusimamishwa kazi kwa Muda usio Julikana.

Kufuatia hatua hiyo kwa nyakati tofauti Wajumbe wa UKAWA wamemlaumu Mwigulu kuwa amesababisha pasaka iwe mbaya kwao. Huyu jamaa utadhani tunalipwa hela zake au hela za CCM. Kwani zake? Kwani za CCM? MJINGA KWELI. HIVI KWANINI ASIFE HUYU? ALISIKIKA MBUNGE MMOJA WA CHADEMA  Mwenye tabia ya maahasira huku akiungwa mkono na wenzake. Baadhi yao  waliwalaumu viongozi wao kwa kusema hakukuwa na sababu ya msingi ya kususa Bunge la Katiba kwa sababu Huruma ya Wananchi waliyoitegemea imekuwa kinyume chake.
"Hapa kiukweli tumejichora. Kumbukeni mwigulu alisema tuna tafuta kujitoa na tunafanya njama ya kuharibu mchakato". Wakati huohuo ikumbukwe Mh:Mnyika baada ya Kushitukiwa kuwa walikuwa na lengo la Kuvuruga Mchakato wa Bunge la Katiba akakanusha akasema Watakuwa wa mwisho kususa bunge au kujitoa au kuvuruga mchakato. Sasa yanefika wapi? Sijui viongozi wao wamesahau? Inakera kweli.
Kwa taarifa za awali hadi sasa Wajumbe 15 wa wanaotoka kundi la 201 wamerejea Bungeni hii leo na Wapo Wajumbe wa CUF klutoka Zanzibar wanajipanga kukutana na Viongozi wao kuomba kurejea kwenye Bunge hilo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top