Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JUMUIYA YA WAISLAM TANZANIA WAMTAKA MH. LUKUVI KUWAOMBA RADHI WAISLAM DHIDI YA KAULI YAKE


Msemaji wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam Tanzania, Rajab Katimba kushoto akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam na kutoa tamko na kumtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, William Lukuvi kuomba radhi Waislam kutokana na kauli aliyoitoa Kanisani wakati wa Bunge la Katiba likiendelea dhidi ya Waislam.
---
SOMA HABARI HII; ILI UWEZE KUJUA CHANZO CHA JUMUIYA YA TAASISI YA KIISLAM TANZANIA KUTOA TAMKO LAO...

April 17 2014 Wajumbe walio upande wa (UKAWA) kwenye bunge la katiba wakiongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba waligoma na kuamua kutoka nje ya bunge hili hapa Dodoma baada ya Profesa Lipumba kumaliza kuzungumza kwamba hawawezi kuendelea na bunge la matusi na ubaguzi.

Kingine kikubwa alichozungumza Prof. Lipumba ni kusikitishwa na kauli ya Waziri Lukuvi aliyoitoa kanisani weekend iliyopita kwamba jeshi litatawala nchi ambapo April 14 2014 gazeti la Mwananchi lilimnukuu Waziri Lukuvi akisema Kanisani‘tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi’

‘Ni kweli kwamba kikao hichi nilipanga nisichangie kwa sababu niliona mechi kali tukishindilia watu watakufa, sikusikia vizuri yaliyotokea jana ila mimi sio mnafiki, nampongeza sana Mh. Mrema kwa hotuba yake juzi, Mrema ndio mpinzani wa kweli, alisema angalia mambo yanayotokea Znz msidhani yataishia Magogoni’

‘Baada ya hotuba ya Rais, mh. Seif Sharrif Hamad alihutubia, yeye ni mchochezi wa hovyo kwa kumsingizia Rais, hakuna mtu yeyote anaweza kunizuia kusema ninayoyaamini mimi, sio hapa wala mtaani, ni kweli Jumamosi nilimwakilisha Waziri mkuu ambae hakunipa hotuba na mambo yalinoga nikatawazwa kuwa chifu’

‘Viongozi wa dini waliliombea Bunge pale Kanisani, mimi Waziri nipo pale… nisiongee chochote??!! tukiendeleza ambayo hayako kwenye mila zetu Znz na Tanganyika inaweza kuwa kama Korea kaskazini na kusini, hofu niliyonayo ni juu ya rasimu yenyewe kwa sababu kwanza imejengwa kwenye misingi ambayo siiamini’

‘Zanzibar inatambulika kama nchi kwenye katiba yao toka hata kwenye katiba ya nyuma kabisa, yapo mapungufu muundo wa serikali 3, ukisoma rasimu wanasema serikali ya Tanganyika imevaa koti la muungano lakini koti lenyewe tunapokezana, leo anavaa Mwinyi, leo anavaa huyu’

‘Hatujawahi kutoa bajeti inayotosha kwa jeshi la Wananchi, mmeshawahi ona wanaandamana kudai haki zao? nina miaka zaidi ya 50 na nisingependa kuiona Tanzania hii inakwenda kwenye maisha ambayo sikuyazoea ili kuepusha haya tusijaribu tusichokijua, hii ni hofu yangu… hakuna wa kunizuia kutoa hofu yangu’

‘Ukweli ni kwamba kama umesoma hii rasimu, muundo unaweza kuwa umeandikwa vizuri lakini hauwezi kuwepo, Rais hakutoa vitisho bali mawazo yake kama Mtanzania, hawa jamaa wamekubaliana, serikali ya Znz wachukue CUF, bara CHADEMA na muungano waachiwe CCM’
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top