Mhe.
Liberata Mulamula akipokewa na mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri
mara tu alipowasili kwenye fundraisng dinner ya Jumuiya ya Watanzania
Columbus, Ohio iliyofanyika Comfort Inn siku ya Jumamosi April 19, 2014.
Mjumbe Michael Mnngodo akiutambulisha uongozi wa Jumuiya kwa Mhe. Balozi Libarata Mulamula na mumewe.
Mjumbe Chiseko Hamisi akielezea mfuko na kazi za mfuko huo na kusisitiza wanajumuiya wajiunge kwa wingi.
Mjumbe Joe Ngwilizi akisoma wasifu wa Balozi Liberata Mulamula.
Mhe.
Balozi Liberata Mulamula akiongea na Watanzania wa Ohio kwa kuwashukuru
kwa makaribisho mazuri waliyompa na kusisitiza upendo na umoja miongoni
mwao pia aliwasifia kwa jitihada zao za kufanya vizuri kwenye maisha kwa
kutimiza malengo yao yaliyowaleta huku ughaibuni. Pamoja na kufanya
fundraising ya mfuko wa Jumuiya kwa ajili ya kutatua matizo yanayotokea
kwenye Jumuiya hiyo, amewaasa kujiandikisha na bima ya WESTADI kwani ni
nafuu sana unalipa $300 tu kwa mwaka au kama unaona haiwezekani tafuta
bima yeyote hata hapa ughaibuni ili kuondoa adha ya michango michango
ambayo wakati mwingine haitimizi malengo na baadae inakuwa usumbufu kwa
wengine na alitolea mfano kwa Mtanzania aliyechomwa Wisconsin kwa sio
utamaduni wetu tumezoea kuzikwa aidha huku au nyumbani, japo kua hata
kuchomwa moto ni gharama pia kwa hiyo ndugu zangu jitahidini muwe na
bima. Mhe. Balozi Libarata Mulamula alijibu maswali ya hapo kwa papo na
maswali mengi yaligusa swala la uraia pacha kwa Wana Columbus kutaka
kujua Ubalozi unasaidiaje swala hilo, Mhe. Balozi aliwajibu kwa
kuwaambia swala la uraia pacha ni swala la wanaughaibuni wote lazima
kuwa kitu kimoja ili kuweza kufanikisha swala hili Ubalozi kupitia
Wizara wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wamelisimia kidedea
swala hili lakini kitu kikubwa ni umoja wenu wa kulipa kipaumbele swala
zima la uraia pacha.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa katibu wa Jumuiya Bi. Happiness Salukele.
Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri.
Meza
kuu kutoka kushoto ni katibu wa jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bi.
Happiness Salukele, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata
Mulamula, Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula na mwenyekiti wa Jumuiya
ya Watanzania Columbus, Ohio Bwn. Jimmy James.
Watanzania waliohudhuria fundraising dinner.
Post a Comment